Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 9 9
kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzungukazunguka, akitafuta mtu ammeze. 9Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani”). Ingawa Agano la Kale halitafuti kukisia sana juu ya somo la ulimwengu wa roho wa giza, ni wazi kwamba baadhi ya mambo yanahusianishwa na kazi ya adui na desturi za ibada ya sanamu, uganga, na nguvu za uchawi (Kum. 32:17; Zab. 96:5). Desturi hizi zilikuwa kinyume na Sheria na mapenzi ya Mungu, zilikatazwa kabisa kwa jamii ya watu wa Mungu (Kum. 18:10-14; 1 Sam. 15:23). Kama msomi mmoja adokezavyo, utendaji wa kipepo katika Agano la Kale unapaswa kueleweka kwa sehemu kubwa kama “nguvu zinazompinga Mungu na viumbe ambao ni watumishi wake, malakim (malaika).” Katika Agano Jipya, maneno yanayohusiana na roho hizi ni daimon na daimonion , uwepo halisi wa viumbe hawa unafafanuliwa kama “-chafu” ( akatharton , Mk 1:24-27; 5:2-3; 7:26; 9:25; Mdo 5:16; 8.7; Ufu. 16:13) na roho “-ovu” ( ponera , Mdo. 19:12-16). Maandiko mengi yanayorejelea shughuli za roho hizi huzihusianisha na kuwatawala watu binafsi. Ingawa Agano Jipya halitafuti kutoa jibu rasmi kuhusu mahali ambapo viumbe hivi vilitokea, hakuna mashaka kwamba vipo katika mawazo ya waandishi wa Agano Jipya, na kwamba vinafanya kazi dhidi ya mambo ya Kristo na kazi yake. Kuna uhusiano mkubwa wa shughuli inayohusiana na viumbe hivi na ibada ya sanamu (rej. Uelewa wa Paulo wa uhusiano kati ya sanamu na mapepo katika 1 Kor. 10:20-21; 12:2; rej. Ufu. 9:20). Paulo na Yohana wanaonyesha kwamba utendaji wa kishetani utaongezeka kadiri mwisho unavyokaribia, huku kukiwa na matokeo yenye nguvu sana ya udanganyifu na upotoshaji wa wengine (1 Tim. 4:1; Ufu. 16:13-14). Wakristo wanapaswa kushughulika na nguvu hizi, kama vile Bwana wetu alivyofanya, kama inavyofafanuliwa katika Waefeso 6:10-18. Mkristo anapaswa kuwa tayari kupambana na “watawala . . . mamlaka. . . nguvu, ulimwengu huu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”
4
M A F U N Z O Y A B I B L I A
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online