Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
9 8 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Haipaswi kukushangaza ikiwa utapata tofauti kubwa ya majibu na maoni kutoka kwa wanafunzi wako kuhusu kutoepukika kwa mateso na upinzani katika maisha ya Kikristo. Kulingana na mlo wa kiroho waliouzoea, wanafunzi wanaweza kuliitikia hili, kwa upande mmoja, kama jambo jepesi tu, na kweli iliyoelezwa waziwazi ambayo ndiyo msingi hasa wa Neno la ushuhuda wa Mungu kuhusu yeyote anayeshirikiana na Masihi. Kwa upande mwingine, ikiwa mlo wa wanafunzi unaelekea kwenye vyakula vya “afya utajiri”, basi mafundisho hayo hayataonekana kuwa yenye manufaa. Yanaweza hata kuonekana kana kwamba ni kuufifisha ushindi Kristo aliotupatia, na mbaya zaidi yanaweza hata kuchukuliwa kama uzushi. Bila kujali mwitikio wa kwanza, ni muhimu kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa jukumu kuu ambalo fundisho hili linatimiza katika mafundisho ya Yesu, na pia kielelezo wazi anachotoa katika maisha yake mwenyewe. Upinzani ambao waumini wanapaswa kuvumilia ni msingi wa utii wao kwa Masihi. Wale wote wanaomchukia watawachukia na wao pia, na lazima wajitayarishe kwa mashambulizi haya na kukataliwa na wale wasiomjua. Hapa tena ni muhimu kufuatilia kwa umakini si tu mgogoro wa kijamii ambao Yesu alikutana nao na watu wa wakati wake katika Israeli, lakini pengine ni muhimu zaidi kufuatilia vita vyake vya mara kwa mara na endelevu dhidi ya majeshi ya kiroho ambayo yalitaka kudhoofisha huduma yake. Shetani na wafuasi wake wana jukumu kubwa katika “filamu” ya Injili, na hakuna ufahamu kamili wa maisha na huduma ya Yesu unaowezekana kufikiwa ambao unapuuza au kudharau nyanja hizi muhimu. Asili ya Mapepo katika Maandiko Ili kuelewa mgogoro endelevu wa Yesu na nguvu za uovu katika enzi hii, unapaswa kutambulisha somo la mapepo kwa wanafunzi kwa ufupi na kwa uangalifu. Ninasema kwa ufupi na kwa uangalifu kwa sababu hatujahimizwa katika Agano Jipya kuwa wataalamu wa njia za “upande wa giza.” Badala yake, tunaambiwa tusiwe wajinga wa hila zake (rej. 2 Kor. 2:11 - “ili tusije tukashindwa na Shetani; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake ”). Kadhalika, tunahimizwa kuwa macho na hila zake kila wakati kwa sababu ya shauku yake ya kummeza mtu yeyote awezaye (k.m., 1 Pet. 5:8-9 – Mwe na kiasi na
4 Ukurasa wa 160 Kujenga Daraja
4
M A F U N Z O Y A B I B L I A
5 Ukurasa wa 161 Muhtasari
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online