Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 0 5

Ufalme wa Mungu Kuzinduliwa kwa Utawala wa Mungu

SOMO LA 1

Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi wa Somo la 1, Ufalme wa Mungu: Kuzinduliwa kwa Utawala wa Mungu . Lengo la somo hili ni kuwapa wanafunzi wako mfumo wa kibiblia ili kuelewa kile ambacho Mungu anafanya katika historia ya mwanadamu, na kuwatayarisha kuwa mashahidi wazuri wa Kristo na Ufalme wake. Somo hili limeundwa ili kuwaonyesha wanafunzi jinsi utawala wa Mungu ulivyokuwa ukipenya ulimwenguni tangu wakati wa Anguko; Mungu hajauacha uumbaji wake, bali amefanya agano la kujiletea watu ambao watakuwa wake milele, kupitia kazi ya wokovu ya Mwana wake, Yesu Kristo. Kwa kujivika mtazamo na tabia ya mpiganaji, Mungu alifanya agano na Abrahamu kubariki familia zote za dunia kupitia ukoo wake, na kwa namna hiyo, Mungu akaamua kurudisha utawala wake duniani. Mungu alifanya upya agano kupitia mababu, watu wake Israeli, kupitia kabila la Yuda na familia ya Daudi. Hatimaye, katika utimilifu wa wakati, Yesu wa Nazareti alitokea, ambaye kuwapo kwake kunawakilisha kutimizwa kwa Ufalme duniani. Kupitia kifo chake, kuzikwa, kufufuka, na kupaa kwake, utawala wa Mungu umekuja kwa nguvu. Wakati utimilifu wa Ufalme bado ni jamblo lijalo, katika Ujio wa Pili wa Kristo, Ufalme wa Mungu umekuja katika nafsi ya Yesu. Theolojia hii ya hali ya juu inawakilisha malengo ya mafundisho ya somo hili, Kuzinduliwa kwa Utawala wa Mungu . Tafadhali, angalia tena katika malengo kwamba kweli hizi zimeelezwa kwa uwazi. Kama kawaida, jukumu lako kama Mkufunzi na mshauri ni kusisitiza dhana hizi wakati wote wa somo, hasa wakati wa majadiliano na muda wa kukaa kwako pamoja na wanafunzi. Kadiri unavyoweza kuangazia malengo katika kipindi chote cha darasa, ndivyo uwezekano wa wanafunzi kufahamu ukubwa wa malengo haya unavyozidi kuwa mkubwa. Ujumbe wa somo la leo ni kuanzishwa kwa Ufalme wa Mungu, si kwa maana ya tukio moja tu, bali katika maana ya maono endelevu, huku kuwapo kwa Yesu Kristo kukiwakilisha kilele cha tangazo la Ufalme. Katika uhalisia, Mungu alianza tangazo la urejesho wa utawala wake duniani na proto-evangelium , tangazo la kwanza la Habari Njema katika Mwanzo 3:15. Katika tangazo la kwamba kichwa cha nyoka kingepondwa na Uzao wa mwanamke, Mungu alitangaza azimio lake la kuleta utaratibu na uzuri katika dunia,

 1 Ukurasa wa 185 Utangulizi wa Somo

1

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

 2 Ukurasa wa 185 Ibada

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online