Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

1 0 6 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

ambayo iliharibiwa na uasi na kutotii kwa mwanadamu na yule mkuu, Ibilisi. Tangazo hili tulivu na lenye uhakika la Ufalme wa Mungu kuwa “karibu” au “kukaribia” linadokeza kwamba kwa kuwapo kwa Yesu ulimwenguni, Ufalme umekuja.

Vipengele vyote vya kujenga Daraja vya somo hili vinahusu kutambua mwanzo na/au kuanza kwa azimio la Mungu la kurejesha Ufalme wake duniani. Wazo la kuanza ni muhimu, sio tu kwa kutambulisha somo, lakini pia litakuwa muhimu kwa matumizi ya kweli za somo katika kipindi hiki. Kwa mfano, kujua kwamba hatua ya kwanza ya Mungu inao msingi katika kazi yake yote ya wokovu ni muhimu katika kutujengea mtazamo wa shukrani kwa Mungu, na pia kuwa na uhakika kwamba tunaamini kazi ya Ufalme ni kazi ya Mungu mwenyewe. Mungu ndiye mfanyakazi, na sisi ni watenda kazi pamoja naye katika mavuno yake, kwa maana “sisi tu wafanyakazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu” (1Kor. 3:9). Mungu ndiye mwigizaji mkuu katika tamthilia ya wokovu, na jukumu letu ni kushiriki pamoja na Mungu kama watenda kazi pamoja katika shamba lake la mizabibu. Kiini hasa cha mifano hii ya kujenga daraja ni kusisitiza masuala ya wanafunzi, bila shaka, lakini kufanya hivyo kwa kuzingatia ukweli huu mkuu. Somo hili linakazia juu ya utambuzi wa kuwapo kwa Ufalme kupitia nafsi ya Yesu wa Nazareti. Hakika, Yesu ndiye Mfalme ambaye nafsi yake ndiyo msingi wa mamlaka yake. Kwa maneno mengine, msingi wa Ukuu na mamlaka ya Yesu unajengwa juu ya asili yake (Yeye ni nani). Kupitia maisha na huduma yake, Yesu wa Nazareti anatekeleza jukumu la Mfalme wa Yehova, awaitaye watu kutoka katika ulimwengu ili wawe milki yake ya pekee (Isa. 55:5; Yn. 10:16, 27). Akiwa Bwana na Mfalme, Yesu amewapa watu wake hukumu na viwango vyake ambavyo vinapaswa kudhibiti utendaji na matendo ya watu wake katika kila njia wanayojitawala (1Kor. 5:4-5; 12:28; Efe. 4:11-12; Mt. 28:19-20; 18:17-18; 1Tim. 5:20; Tit. 3:10). Kwa uwezo na mamlaka yake ya kifalme Yeye hulinda, hutegemeza, na kuhifadhi watu wake katikati ya dhiki, migogoro, na majaribu kwa ajili ya jina lake (2 Kor. 12:9-10; Rum. 8:35-39); na kupitia mamlaka yake ya kifalme aliyopokea kutoka kwa Baba yake, yeye kama Bwana

 3 Ukurasa wa 186 Kujenga Daraja

1

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

 4 Ukurasa wa 187 Muhtasari

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online