Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 0 7

hushinda, hushikilia, na kuusimamia uwezo wake ili kupunguza ushawishi na athari za adui zake (Mdo. 12:17; 18:9-10; 1Kor. 15:25). Akiwa ndiye aliyeteuliwa na Mungu kuwa na mamlaka yote mbinguni na duniani, yeye huamuru na kupanga vitu vyote viwepo kwa ajili ya utukufu na heshima yake kuu zaidi, na huamua wema wa asili katika mambo yote (Rum. 8:28; 14:11; Kol. 1:18; Mt. 28:19 20). Naye akiwa Hakimu, siku moja atatekeleza hukumu ya haki ya Baba juu ya wale wote wanaokataa habari njema ya Ufalme, na yeye mwenyewe atalipiza kisasi juu ya wale wanaokataa utawala wake na kuasi Injili yake (Zab. 2:9; 2 The. 1:8) Kuingia kwa Yesu ulimwenguni kunawakilisha kiwango kipya cha makali na umakini kwenye vita ya kiungu ya Bwana ya kurejesha utawala wake ulimwenguni. Kiuhalisia, Yesu wa Nazareti anazidisha makali ya vita vya Ufalme ulimwenguni kwa kuelekeza nguvu kubwa sana si dhidi ya dhambi na uovu wa wanadamu, bali dhidi ya nguvu ovu za yule Mwovu, na mamlaka na enzi katika ulimwengu wa roho. Yesu anaanzisha Ufalme kwa nguvu ya kweli dhidi ya ufalme wa shetani, lakini hapigani vita kwa mkuki na upanga, bali kwa silaha za vita vya rohoni katika Roho Mtakatifu. Kwa mfano, Petro anapoamua kutumia upanga kumlinda Yesu, anamkemea na badala yake anakwenda msalabani, ambayo ndiyo silaha kuu ya siri ya Ufalme wa Mungu (Mt. 26:50-56). Dhana hii ya Yesu kama Shujaa Mkuu na kifo cha Kristo msalabani kama silaha kuu inaelezewa na Paulo katika Wakolosai ambapo anazungumza juu ya kifo cha Yesu kama kunyang’anya enzi na mamlaka (Kol. 2:15), na kushindwa kabisa kwa enzi na mamlaka hizo kupitia msalaba. Kifo na kupaa kwa Yesu linachukuliwa kama aina ya sherehe ya ushindi, gwaride la Jenerali Mkuu ambaye ameleta nyara na wafungwa wa vita katika gari-moshi la Mshindi wake hodari. Wazo hili linaweza kuonekana pia katika Waefeso 4:7-8, pamoja na nukuu yake kutoka Zaburi 68, wimbo wa kawaida wa vita vya kiungu. Katika namna ya ajabu, Bwana wetu Yesu aliwashinda maadui wa Mungu na kuzindua Ufalme, akishinda vita kubwa kuliko zote msalabani, kwa kuuawa, si kwa kuwaua wengine kimwili.

1

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

 5 Ukurasa wa 188 Muhtasari wa Kipengele I

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online