Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
1 0 8 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Kwa namna fulani Yesu anaweka katika kuja kwake kielelezo na kiwango cha vita vyote halali vya kiroho. Tunamshinda adui si kwa kuangamiza maisha ya wengine, bali kwa kutoa maisha yetu kwa ajili yao; tunashinda vita dhidi ya maadui wa Mungu si kwa kuua wanadamu, bali kwa kuishi kama dhabihu iliyo hai, inayokubalika kwa Mungu (Rum. 12:2; Yn. 12:25). Tunashinda si kwa uwezo wa bunduki, kisu na kombora, bali kwa Neno la Mungu na ngao ya imani (Efe. 6:10-18). Kitendo cha Yesu kumshinda adui kunathibitisha kwamba sehemu kubwa ya vita inahusika na mapambano yetu binafsi ya ndani dhidi ya uovu uliobaki ndani (Rum. 7:7-25; 2 Kor. 10:1-6). Wazo hili, la kwamba kupitia kuja kwa Yesu Kristo Ufalme ulifunuliwa wazi katika ulimwengu, ni ufunuo muhimu katika utimilifu wa ahadi ya kiagano ya Mungu ya kurudisha utawala wake duniani. Pamoja na Yesu tunapitia uzoefu wa enzi ya Kimasihi katika uhalisia wake, si tu kama wazo au tumaini au shauku, lakini katika ukweli halisi. G. E. Ladd anaweka hoja hii kwa uwazi anaposema: Yesu alitangaza kwamba Ahadi hii [Ahadi ya kuja kwa Ufalme] hakika ilikuwa inatimizwa. Huu sio Ufalme wa kimaono bali ni wokovu wa sasa. Yesu hakuwaahidi wasikilizaji wake hatima bora zaidi au kuwahakikishia kwamba wangeingia katika Ufalme hivi karibuni. Badala yake alitangaza kwa ujasiri kwamba Ufalme ( Herrschaft , yaani utawala) wa Mungu ulikuwa umewajia. Kuwapo kwa Ufalme kulikuwa “tukio, tendo la neema la Mungu.” Ahadi hiyo ilitimizwa katika kazi ya Yesu: katika kuwatangazia maskini habari njema, kufunguliwa kwa wafungwa, kuwarudishia vipofu uwezo wa kuona, kuwafungua walioonewa. Hii haikuwa theolojia mpya au wazo jipya au ahadi mpya; lilikuwa ni tukio jipya katika historia. “Wanyonge wanasikia habari njema, milango ya gereza iko wazi, waliokandamizwa wanapumua hewa ya uhuru, wasafiri vipofu wanaona nuru, siku ya wokovu imefika.”
1
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
6 Ukurasa wa 189 Muhtasari wa Kipengele I-D
~ G. E. Ladd. The Presence of the Future. Grand Rapids: Eerdmans Publishing, 1974. uk. 111-112.
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online