Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 0 9

Kwa kuzingatia yale yote ambayo Yesu wa Nazareti aliyatimiza kupitia kifo, ufufuo, na kupaa kwake, kazi yake kama Shujaa wa Kiungu katika kuanzisha Ufalme wa Mungu bado haijakamilika. Usomaji rahisi wa kitabu cha Ufunuo na sehemu nyingine za kinabii za Agano Jipya unadhihirisha kwamba atatimiza huduma aliyoianzisha katika maisha yake, kifo, ufufuo na kupaa kwake. Yesu mwenyewe alizungumza juu ya siku kuu ambayo yeye kama Mwana wa Adamu angekuja juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na malaika watakatifu ili hatimaye na kwa ukamilifu apate kuzishinda nguvu zote ambazo zingepinga mapenzi yake (Mk. 13:26). Maono haya na lugha hii vinaakisi maono makuu ya nabii Danieli, ambaye anamzungumzia mtu kama huyo katika Danieli 7:13. Ufalme wa Mungu unakuja kwa nguvu, kama vile Yohana Mbatizaji alivyotabiri ungekuja. Bwana wetu, ambaye alikuja mara ya kwanza kutekeleza silaha ya siri ya Mungu ya msalaba juu ya adui zake, kwa kweli atarudi tena, wakati huu akiwa Shujaa wa kweli wa Kiungu ambaye kazi yake ni ya wazi, kamilifu, na yenye uharibifu kwa adui zake. Ufunuo 19:11-16 inaeleza ujio wa Bwana wetu Yesu Kristo katika taswira ya Shujaa wa Kiungu; anakuja juu ya farasi mweupe, aliyevikwa vazi liliyochovywa katika damu, na upanga wenye makali kuwili ukitoka kinywani mwake. Nyuma yake kuna majeshi kamili ya mbinguni “anapohukumu na kufanya vita” (mstari 11). Maono ya mwisho ya Biblia kuhusu Yesu kama Shujaa wa Kiungu wa Mungu yanamalizia ufunuo huo kwa taswira ya ajabu ya vita vya mwisho, ambavyo, kwa uchache sana, lazima viwe ishara toshelevu na yenye nguvu ya hukumu ya mwisho na ya kisasi inayokuja na ghadhabu ya Mungu aitoayo kwa wale ambao wamepinga utawala wake bila kutubu. Katika uhalisia, Yesu wa Nazareti ndiye Mpakwa Mafuta, aliyechaguliwa na Mungu ili kukomesha pambano lililoanza na uasi wa nyoka na kutotii kwa wanadamu wawili wa kwanza. Ni yeye ambaye atamponda-ponda kakos , yule ambaye kupitia uwongo na udanganyifu wake alileta taabu na mateso juu ya dunia (Rum. 16:20; Ufu. 12:9), na ambaye anawakilisha aina mbaya zaidi ya upinzani wa ukaidi kwa utawala wa Mungu. Ahadi ya Mwanzo 3:15 hatimaye imetimia katika nafsi ya Mnazareti mpole, anayefanya vita vya Mungu, si kwa kuua bali kwa kufa na kufufuka tena kwa niaba ya wale aliokuja kuwaokoa.

 7 Ukurasa wa 195 Hitimisho

1

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online