Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

1 1 0 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

Lengo la maswali haya katika kipengele hiki sio kukufanya uhisi hitaji la kulipitia kila moja. Sio tu kwamba hili litakuwa jambo gumu na la kuchosha, linaweza pia kukuondoa katika kuzingatia masuala mengi magumu na muhimu ya wanafunzi wako. Ingawa maswali haya yanakusudiwa kukusaidia kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa dhana zilizoonyeshwa kwenye video, itabidi uweke uwiano kati ya lengo hilo na lengo dhahiri la kushughulika na maswali na mambo yale wanayovutiwa nayo wanapoitikia Maandiko na nyenzo zingine. Mojawapo ya malengo katika kuangazia mifano halisi katika somo hili ni kufanya muunganisho maalum na muhimu wa yale mambo ya kieskatolojia ambayo bila shaka ni magumu sana na utendakazi wa vitendo wa huduma katika jiji. Mojawapo ya mambo yenye changamoto zaidi kwa wanafunzi kufanya ni kuona uwiano kati ya mafundisho ya maandiko juu ya Ufalme na maisha yao wenyewe na huduma. Iwapo unatumia au hutaki kutumia mfano halisi hapa chini au utachagua kubuni tukio lako mwenyewe la kujadili, lazima utafute kufanya muunganiko kuwa wazi kati ya kile ambacho wanafunzi wamesikia, kujifunza, na kujadili, na kile wanachokabiliwa nacho katika huduma zao. Kwa kuzingatia hili, mfano wa hapa chini unajaribu kuchukulia kwa uzito kile ambacho kingetokea ikiwa kunaweza kuwa na msisitizo usiofaa au uliotiwa chumvi juu ya Ufalme kama jambo lililopo tayari, au kama ungechukuliwa kuwa jambo la wakati ujao tu. Amini usiamini, jinsi mhudumu wa mijini anavyoitazama theolojia hii itakuwa na athari kubwa juu ya namna atakavyoiendea huduma na kuendelea katika kazi yake kwa ajili ya Bwana. Usichukulie kuwa ni jambo la kawaida sana au lisilo la lazima kuwauliza wanafunzi kama wanahitaji maombi kwa ajili ya mtu fulani au kitu kinachohusiana na mawazo na kweli zinazofundishwa katika somo. Maombi ni njia ya ajabu ya kutumia kweli kwa njia ya vitendo na yenye manufaa; kupitia kupeleka mahitaji maalum kwa Mungu kwa kuzingatia ile Kweli ya Neno la Mungu, wanafunzi wanaweza kuimarisha mawazo hayo katika nafsi zao, na kupokea tena kutoka kwa Bwana majibu wanayohitaji ili kutegemezwa katikati ya huduma zao.

 8 Ukurasa wa 195 Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu

1

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

 9 Ukurasa wa 198 Mifano Halisi

 10 Ukurasa wa 199 Ushauri na Maombi

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online