Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 1 3

Mungu Baba Mungu wa Utatu – Ukuu wa Mungu

SOMO LA 2

Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi wa Somo la 2, Mungu Baba: Mungu wa Utatu – Ukuu wa Mungu. Tutalitambulisha wazo la Utatu kwa wanafunzi wako, yaani dhana ya kibiblia inayohusiana na asili ya utatu wa Mungu kama Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Hili haliwezi kushughulikiwa kikamilifu katika muda tuliopewa katika somo kwa njia ya video. Hata hivyo, kinachowezekana ni kwamba tunatoa muhtasari wa muundo wa masuala makuu yanayohusiana na mafundisho yote haya mawili yenye uhusiano wa karibu ambayo yatawawezesha wanafunzi kuendelea na utafiti wao wa masomo haya muhimu katika miezi na miaka ijayo. Unapowaongoza wanafunzi wako katika fundisho la Utatu, zingatia akilini mawazo manne rahisi ambayo yanaweza kukuongoza unapojadili fundisho hili muhimu pamoja nao. Kwanza, kumbuka kwamba Mungu ni Mungu mmoja . Hakuna Miungu wawili katika Biblia, mmoja katika Agano la Kale na mwingine katika Agano Jipya. Mungu yuleyule yumo katika maagano yote mawili, na asili ya Mungu inapata udhihirisho kamili na wa kina zaidi katika Agano Jipya kupitia Yesu Kristo, ambaye ametupatia ujuzi kamili na wa kina kumhusu Baba (rej. Yn. 1:14-18). Pili, Mungu anajidhihirisha kwetu katika nafsi tatu tofauti na zote zinahusika katika tukio la wokovu, na bado Mungu anabaki kuwa umoja usiogawanyika. Kama utakavyoona, unapochunguza maandiko yaliyomo katika somo hili, kwamba Baba anajidhihirisha katika Mwana na Roho pasipo kwa njia yoyote kuchanganya nafsi pamoja nao, au wao kuchanganya nafsi zao na ile ya Baba. Uungu ni utofauti na bado ni umoja. Tatu, tunaweza kuuelewa Utatu katika namna bora zaidi tunapoelewa jukumu la kila nafsi katika mpango wa wokovu . Baba anakusudia, Mwana anatekeleza, na Roho anaachilia baraka ya ukombozi kwa mwamini na katika Kanisa. Agano Jipya halikisii kwa habari ya kiini cha Uungu, bali linaonyesha kile ambacho kila nafsi inafanya kuhusiana na wokovu tulioupata kwa njia ya Kristo. Nne, fundisho la kimaandiko la Utatu haliwezi kupimwa kwa kugeukia mantiki na uchambuzi pekee; kwetu linabaki kuwa fumbo kabisa. Ingawa kumekuwa na majaribio mengi ya kuweka wazi maana ya fundisho la Biblia la Utatu, haipasi kutushangaza kwamba hakuna maelezo ya kibinadamu yanayoweza kutoa ufahamu wa kina wa

 1 Ukurasa wa 201 Utangulizi wa Somo

2

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online