Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
1 1 4 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
utukufu na adhama ya asili ya nafsi za Uungu, yaani Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Wewe na wanafunzi wako mnapochunguza Neno la Mungu katika somo hili, ninaamini kwamba mtaweza kudhihirisha unyenyekevu wenu na bidii yenu katika somo hili. Bila shaka, vyote viwili vitahitajika! Ibada hii inalenga Fumbo Kuu katika kutafuta kumwelewa Bwana kama Umoja wa Utatu. Ingawa neno utatu halipatikani katika Biblia, limekuwa neno lililobuniwa ili kuelezea fundisho la Maandiko kuhusu umoja wa Mungu unaoishi katika Nafsi tatu tofauti. Neno hili linatokana na neno la Kiyunani trias , na lilitumiwa kwanza na Theophilus (168 183 BK). Matumizi mengine yalitoka kwa mtetezi wa imani ya Kikristo, Mkristo na wakili Tertullian (220 BK), ambaye alikuwa wa kwanza kutumia neno la Kilatini trinitas kuelezea fundisho hili. Ijapokuwa katika zama za baada ya Biblia waamini wa Kanisa walijaribu kuelezea fundisho la Umoja wa Utatu wa Mungu kwa maneno na lugha yenye ushawishi na ya kimantiki kifalsafa, matumizi ya mawazo mbalimbali ya Kiyunani yaliwasaidia baadhi tu katika kupata maana ya asili ya Mungu. Inaonekana Kanisa limeelekea kuhama kutoka kwenye maungamo ya wazi ya Agano Jipya juu ya jinsi Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu wanavyotenda kazi katika wokovu hadi kwenye mijadala isiyoeleweka zaidi kuhusu asili sahihi ya utendaji wa ndani kabisa wa Uungu. Ingawa jitihada hizo ni za kishujaa, haziwezi kutoa ufahamu wa mwisho wa Utatu. Ninaamini kwamba ipo njia nyingine, njia rahisi zaidi. Tunaweza kutumia njia ya imani na kulipokea fundisho hili kama fumbo. Utatu kama fundisho si matokeo ya kujaribu kutumia mawazo ya Kiyunani kumfafanua Mungu wa Abrahamu. Badala yake, linatokana na kuzing’ang’ania maana za Maandiko ya Agano la Kale na Agano Jipya zinazomzungumzia Mungu ambaye amejidhihirisha katika nafsi tatu: Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, na bado kwa namna yoyote hajitaji kuwa Yeye ni miungu mitatu, au kama Mungu mmoja achukuaye maumbo matatu tofauti kwa ajili ya makusudi mbalimbali. Mungu huyu mkuu wa Maandiko amejifunua katika Kristo, ambaye kwa Roho Mtakatifu alitimiliza makusudi ya Baba yake kwa ajili ya kuokoa ulimwengu.
2 Ukurasa wa 201 Ibada
2
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online