Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 1 5
Ushuhuda wa Daudi katika Zaburi ndogo ya 131 ni mgodi halisi wa dhahabu wa ufahamu kwa ajili yetu tunapotafuta kuzama ndani ya kina cha nafsi ya Bwana mwenyewe: Zab. 131:1-3 – Bwana, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala na mambo yashindayo nguvu zangu. 2Hakika nimeituliza nafsi yangu, Na kuinyamazisha. Kama mtoto aliyeachishwa Kifuani mwa mama yake; Kama mtoto aliyeachishwa, Ndivyo roho yangu ilivyo kwangu. 3Ee Israeli, umtarajie Bwana, Tangu leo na hata milele. Hebu basi tusisitize lugha ya Biblia iliyowazi kabisa: Mungu ni mmoja. Kum. 6:4 – Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja 1 Fal. 8:60 – . . . Watu wote wa ulimwengu wajue ya kuwa Bwana ndiye Mungu; hakuna mwingine. Isa. 44:6 – Bwana, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, Bwana wa majeshi, asema hivi; “Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu.” Lakini wacha pia tuweke msisitizo kwamba Yesu ni Neno aliyefanyika mwili (Yn 1:14), na tumthibitishe Roho Mtakatifu kama Bwana na mpaji wa uzima kwa Kanisa (2 Kor. 3:17-18). Na tuwaruhusu waandishi wa vitabu vyetu vya kiada kuwa na neno la mwisho hapa: Kainisa halijasita kufundisha fundisho la Utatu. Bila kujifanya kwamba linaelewa, limetoa ushahidi wake, limerudia yale ambayo Maandiko Matakatifu yanafundisha. Baadhi wanapinga wakisema kwamba Maandiko hayafundishi Utatu wa Mungu kwa msingi kwamba wazo zima la Utatu katika umoja ni mkanganyiko wa maneno; lakini ikiwa hatuwezi kuelewa kuanguka kwa jani kando ya barabara au kuanguliwa kwa yai la ndege kwenye kiota kule, kwa nini Utatu uwe tatizo kwetu? “Tunamfikiria Mungu kwa kiwango cha juu zaidi” anasema Michael de Molinos, “kwa kujua kwamba yeye hawezi kueleweka, na yuko juu ya ufahamu wetu, kuliko
2
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online