Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 1 7
Mtu anaweza kujua mengi juu ya Mungu bila kumjua sana. Nina hakika kwamba wengi wetu hatujawahi kulielewa hili. Tunapata ndani yetu shauku kubwa katika theolojia (ambayo, bila shaka, ni elimu ya kuvutia zaidi – katika karne ya kumi na saba ilikuwa ni jambo ambalo kila mwanaume mstaarabu alilipenda). Tunasoma vitabu vya ufafanuzi na utetezi wa kitheolojia. Tunatazama katika historia ya Kikristo na kujifunza ukiri wa imani ya Kikristo. Tunajifunza kutafuta mambo mbalimbali kuhusiana na Maandiko. Wengine wanathamini kupendezwa kwetu na mambo haya, na tunajikuta tunaombwa kutoa maoni yetu hadharani juu ya swali hili au lile, kuongoza vikundi vya kusoma, kujadili kuhusu mada mbalimbali za kazi za kitaaluma, kuandika makala, na kwa ujumla kukubali kuwajibika, kwa njia rasmi au isiyo rasmi, kwa kutenda kama walimu na waamuzi kwa habari ya kipi ni halisi na sahihi na kipi sio katika jamii yetu ya Kikristo. Rafiki zetu hutuambia namna wanavyothamini mchango wetu, na hilo hutuchochea kuchunguza zaidi kweli ya Mungu, ili tuweze kuendana na kukidhi mahitaji tunayotwishwa mabegani mwetu. Yote ni sawa – lakini kupendezwa na theolojia, na maarifa juu ya Mungu, na uwezo wa kufikiria wazi na kuzungumza vizuri juu ya mada za Kikristo, sio kitu sawa na kumjua Yeye. Tunaweza kujua mengi kuhusu Mungu kama Calvin alivyojua – kwa hakika, ikiwa tutajifunza kazi zake kwa bidii, mapema au baadaye tutajifunza – na bado wakati wote (tofauuti na Calvin, naomba niseme) tukawa hatumjui Mungu hata kidogo. Wakumbushe wanafunzi kwamba kile kilicho hatarini katika kujifunza Utatu ni ufahamu wetu halisi wa Mungu jinsi alivyojifunua kwetu . Maana yake ni kwamba kila kitu kiko hatarini tusipojifunza namna Mungu alivyo. Kauli za Tozer kuhusu Utatu ni za kweli leo kama wakati wa kwanza alipofikiria na kuandika maneno yafuatayo: Fundisho la Utatu ni ukweli kwa ajili ya moyo. Ni roho ya mwanadamu pekee inayoweza kuingia kupitia pazia na kupenya ndani ya Patakatifu pa Patakatifu. “Acha nikutafute kwa kutamani” Anselm alisihi, “nikutamani katika kukutafuta; acha nikupate katika ~ J. I. Packer. Knowing God . Downers Grove: InterVarsity Press, 1993. uk. 26.
2
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
4 Ukurasa wa 215 Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online