Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

1 1 8 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

upendo, na kukupenda katika kukupata.” Upendo na imani vimetulia katika fumbo la ajabu za Uungu. Wacha ufahamu wa kawaida upige magoti kwa heshima hadharani.

~ A. W. Tozer. The Knowledge of the Holy. New York: Harper San Francisco, 1961. uk. 20.

Mjadala wako kuhusu kweli za Utatu haupaswi kujikita katika kujaribu kutatua fumbo la Uungu, badala yake ujikite katika kuelewa “uelekeo,” kwa maneno mengine, wa elimu ya kibiblia na kitheolojia kuhusu Utatu. Zingatia mambo makuu ya fundisho la Utatu: umoja wa Mungu, nafsi tatu zinazoshiriki asili moja katika Uungu, utofauti wa washiriki wa Utatu. Kwa kuzingatia mambo makuu unaweza kuweka mfumo ambao si tu kwamba utawasaidia wanafunzi kufahamu taarifa hizi, lakini pia utawapa njia ya kujifunza somo hili muhimu katika siku zijazo. Mifano hii halisi imekusudiwa kuchunguza umuhimu wa imani katika Mungu kama Utatu kwa ajili ya maisha na huduma. Wasaidie wanafunzi wafikirie kile kilicho hatarini katika kukana ukweli wa Maandiko kuhusu nafsi ya Mungu, na uwasaidie kufafanua mipaka ya kile kinachoonwa kuwa kinakubalika kwa habari ya maoni mbalimbali kuhusu Utatu. Kufikia mwisho wa somo la pili, unapaswa kuwa umewaeleza wanafunzi hitaji la wao kuwa wamefikiria na kufanya kazi ya msingi kwa ajili ya Kazi ya Huduma kwa Vitendo. Sasa, kufikia mwisho wa somo la tatu, unapaswa pia kuwa umesisitiza haja ya wao kuchagua kifungu kwa ajili ya Kazi yao ya Uchambuzi wa Maandiko (eksejesia). Kazi hizi zote mbili zina kawaida ya kuwashitukiza wanafunzi mwishoni mwa kozi, kwa hiyo hakikisha unawasisitiza kuhusu kazi zinazopaswa kufanywa, viwango vya kuzingatia wanapozifanya, na tarehe ambayo kazi zinatarajiwa kukamilika. Wape taarifa stahiki kuhusu kazi zao za mwisho na kazi nyingine zozote husika, na uwasihi wajipange na kuwa tayari kwa kazi hiyo kubwa iliyo mbele yao.

2

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

 5 Ukurasa wa 217 Mifano Halisi

 6 Ukurasa wa 220 Kazi

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online