Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

1 2 2 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

na kufanya njia ya ghadhabu yake ya kimungu kutoshelezwa na huruma yake kumwagika hata juu ya wamataifa wenye hatia (Rum. 3). Kwa kifo chake tumesamehewa dhambi zetu (Kol. 2:13) na dhambi zetu zilitupwa mbali nasi kupitia kifo cha Kristo kwa ajili yetu (cf. Mt. 6:12; 9:6; Yak. 5:15; 1 Yoh. 1:9). Sasa tumehesabiwa haki kwa njia ya kifo chake, na tuna amani na Mungu kwa njia ya imani katika Yesu (Rum. 5:1). Pamoja na haya yote na taswira nyingine zinazoonyesha utajiri uliopatikana kwa ajili yetu kupitia kifo cha Kristo, itakuwa muhimu kwako kuwa kielelezo cha sifa muhimu ya kuwa na majibu mengi sahihi kuhusiana na kifo cha Mwana wa Mungu kwa ajili yetu. Katika mjadala na mwenendo wako, kuwa kielelezo cha umuhimu wa kuchukua njia ya kupatanisha kweli zote muhimu kuhusiana na maana ya kifo cha Kristo. Mambo mengi yametimizwa na Bwana wetu, na lengo letu linapaswa kuwa kuwawezesha wanafunzi wetu kutambua na kusherehekea ukweli huu muhimu. Kama kawaida, zingatia kwa makini malengo ya somo hili. Yatakusaidia kukuongoza katika aina ya ufahamu wa utajiri wa Kristo ambao unahusishwa na mateso yake kwa niaba yetu. Ibada hii inaangazia asili ya kifo cha Bwana wetu kama mbadala , ambayo ni muhimu sana ili kuelewa ushiriki wetu katika kifo cha Kristo, na kuendelea kubeba msalaba wetu mbele zake. Kristo hakufa katika ombwe au bila sababu wala kusudi; kifo chake kilikuwa adhabu ya moja kwa moja juu ya nafsi yake ya kiungu kwa sababu ya matendo yale yale ambayo tumetenda mara elfu nyingi sana. Uasi wetu , kutotii kwetu , upumbavu wetu , na ukatili wetu ndio uliomfanya avumilie kukataliwa na ghadhabu ya Baba yake badala yetu. Mara nyingi, inawezekana kugeuza kifo cha Yesu kuwa mazungumzo ya kufikirika kuhusu masuala ya kitheolojia, mawazo potofu kuhusu mambo ambayo akili ya mwanadamu haikukusudiwa kuyafahamu kamwe. Badala ya kukumbatia maana iliyo wazi na ya moja kwa moja ya Maandiko, tunaficha ushiriki wetu katika mateso na mauaji ya Kristo kwa kuyafunika kwa maneno makubwa kuhusu “upatanisho” na “kuhesabiwa haki.” Wakati, kwa kweli, nywele zake ziling’olewa, alipigwa ngumi usoni, na mgongo wake ukachanwa kama utepe kwa mijeledi kwa sababu ya hatia yetu wenyewe mbele za Mungu.

3

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

 2 Ukurasa wa 223 Ibada

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online