Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 2 3

Tumeikanyaga sheria ya Mungu, na kifo chenye uchungu cha Yesu kilikuwa jibu lake la upendo kwa matendo yetu. Kupitia kifo cha Yesu, dhambi yangu binafsi imesamehewa. Tafakuri ya aina hii mara moja inafunua kusudi halisi la ujuzi wa Kristolojia: ibada na upendo wa Mungu wetu mkuu na Baba yetu, kwa njia ya Yesu Kristo. Upendo wa Mungu usiopimika, wa milele na wa ajabu ulionyeshwa kwa kupigwa kikatili, kupigwa mijeledi, kufedheheshwa, na hatimaye kifo cha kutisha cha Bwana wetu msalabani. Ajabu ya upendo wa Mungu haipaswi tu kusababisha uandishi wa insha zinazong’aa kwenye karatasi nyeupe, bali roho zilizovunjika, zilizonyenyekezwa mbele za Mungu na tayari kutumika kwa njia ile ile ambayo Bwana wetu mpendwa alijinyenyekeza na kuwa mtiifu hadi kifo, naam, kifo cha msalaba. Jaribu kuweka wazi hisia za kina na lugha ya moyo hapa, na sio tu katika ibada hii, lakini katika somo zima. Wawezeshe wanafunzi wako kuona na kuhisi tendo hili la kutisha lilivyokuwa wakati Bwana wetu mpendwa alipojiweka mahala petu na kubeba maovu na uasi ambao tumedhihirisha pasipo kujali na kwa upumbavu tangu utotoni. Hakika Bwana wetu alikufa kwa sababu Baba alimtwisha maovu yetu sisi sote . Kipengele cha Kujenda Daraja katika somo hili kimeundwa ili kusaidia kukazia ufahamu wetu kuhusu ukweli na maana za kifo cha Kristo. Hili ni mojawapo ya kazi muhimu zaidi, na ngumu hata hivyo, kwetu kama watu tunaolea na kukuza viongozi. Je, ni kwa namna gani na kwa njia zipi tunawasaidia viongozi wa Kikristo wanaoinukia kugundua tena maana ya kifo cha Yesu, wakati katika mazingira mengi sana kifo hicho kimepuuzwa, kimechukuliwa kidhahania kupita kiasi, na kwa hakika kupunguzwa umuhimu wake kama kiini cha imani na maisha ya Kikristo, katika suala la kazi yake ya msingi , iliyoleta wokovu na ukombozi wetu, na kazi yake ya kibinafsi , yaani, wajibu wetu wa kuchukua msalaba wetu na kumfuata, tukifananishwa na kifo chake ? Unapoendelea katika somo hili, kuwa mwangalifu hasa kwa janga la siku hizi la aina ya ufahamu usio makini (badala ya ufahamu makini) wa kifo cha Yesu. Lengo letu lazima liwe kusaidia

3

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

 3 Ukurasa wa 226 Kujenga Daraja

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online