Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
1 2 4 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
kutambulisha tena Kweli hii muhimu kwa uwazi na upya, ili wanafunzi wetu waweze kuona taswira ya Bwana kama aliyesulubiwa mbele yao. Paulo anaonyesha kwamba hili linawezekana katika ukosoaji wake wa ugonjwa wa Galatia wa kupuuza maana kubwa ya kifo cha Kristo kwa ajili ya wokovu na ufuasi. (Gal. 3:1 - Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?) Maswali hapa chini yanatafuta kuangazia tena dhana muhimu zinazohusiana na Kristo na kifo chake, ambazo ziliwasilishwa katika sehemu ya kwanza ya video. Ufafanuzi wa AJ wa maana na njia ya kifo cha Kristo msalabani unajumuisha aina mbalimbali za ajabu za taswira muhimu ambazo lazima uwasaidie wanafunzi wako kuzielewa na kuzijadili katika sehemu hii ya moduli. Sehemu kadhaa za Maandiko zimeingiliana na zinafafanua mifano hii, ikijumuisha maandiko kama vile 2 Wakorintho 5:14-6:2 na Warumi 3:24-26. Warumi 6:1-11 inazungumza hata juu ya kushiriki kwetu katika kifo chake, kufisha miili yetu, na kushiriki kwetu katika ufufuo unaodhihirishwa katika kuishi maisha mapya. Unachopaswa kutafuta kufanya katika mjadala huu ni kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa muhtasari mkuu wa taswira muhimu za Agano Jipya kuhusu asili ya kifo cha Kristo, na manufaa ya msingi ambayo muhtasari huu ulitoa. Katika sehemu inayofuata, taswira hizi zitazingatiwa kwa kina zaidi na kwa kuzingatia mahala pake kihistoria. Unachopaswa kuwasaidia wanafunzi wako kuelewa katika sehemu hii ni utajiri wa taswira zinazohusishwa na kazi ya Kristo msalabani na manufaa yake. Mwenendo wa wanatheolojia wachanga wa kupunguza (kutafsiri kila kitu katika mtazamo mmoja) na kuwa watu wasio na hisani (kushindwa kuwaheshimu na kuwasikiliza wale walio na maoni tofauti) ni tabia ambayo lazima tujihadhari nayo kila wakati. Ni vyema tujitahidi kuwawezesha kuwa na mioyo iliyo wazi (tayari kuona zaidi ya upande mmoja wa suala) na kuweza kuahirisha hitimisho (mpaka misimamo yote isikilizwe na kueleweka).
4 Ukurasa wa 237 Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu
3
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
5 Ukurasa wa 239
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online