Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 2 5
L. L. Morris anatupatia muhtasari mzuri wa utajiri wa mtazamo wa kibiblia kuhusu kazi ya upatanisho ya Kristo katika Maandiko. Kazi ya upatanisho ya Kristo inatazamwa katika mitazamo kadhaa. Hivyo, wenye dhambi ni watumwa wa dhambi zao (Yohana 8:34), lakini Kristo amewaweka huru (Gal. 5:1). Walishikwa katika dhambi ya Adamu: “katika Adamu wote wanakufa” (1Kor. 15:22). Lakini Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu (1 Kor. 15:3) na madhara ya dhambi ya Adamu yamebatilishwa (Rum. 5:12-21). Wenye dhambi wako chini ya hukumu, hukumu ya hapa na ya sasa (Rum. 1:24, 26, 28) na hukumu ya mwisho wa nyakati (Rum. 2:16), lakini hakuna hukumu kwa wale walio katika Kristo (Rum. 8:1). Tu mateka wa sheria ya dhambi (Rum. 7:23), wakati kwa upande mwingine hakuna mtu atakayehesabiwa haki kwa matendo ya sheria (Rum. 3:20). Lakini tumefunguliwa kutoka katika utumwa wa Sheria, tumeifia ile sheria iliyotufanya tuwe watumwa (Rum. 7:4). Ni kweli kwamba ukweli kuhusu ghadhabu ya Mungu kudhihirishwa kwa wenye dhambi ni fundisho ambalo limeepukwa kwa bidii katika sehemu kubwa ya theolojia ya kisasa; hata hivyo, hilo haliondoi ukweli kwamba fundisho hilo liko wazi katika Agano Jipya (Luka 3:7; Yoh. 3:36; Rum. 1:18; 2:5; nk.). Lakini pia kuna fundisho la wazi kwamba Kristo amegeuza hasira hiyo kutowaelekea wenye dhambi (1 Thes. 1:10; 5:9). Hii ndio maana ya upatanisho pia (Rum. 3:25; 1 Yoh. 2:2). Kifo ni dhalimu mwingine (Rum. 6:23) ambaye Kristo ametuweka huru dhidi yake (Rum. 5:17; 1 Kor. 15:52-57). Mwili ni mwovu (Gal. 5:19-21; Efe. 2:3), lakini umesulubishwa kwa wale walio wa Kristo (Gal. 5:24). Kuna ubatili kuhusu mambo mengi ya maisha katika ulimwengu huu, lakini Wakristo wamekombolewa kutoka humo (Rum. 8:20-23); maisha yao si bure (1Kor. 15.58; Flp. 2:16). ‘Ulimwengu’ ni adui wa Kristo (Yohana 7:7; 15:18), lakini ameushinda (Yohana 16:33). Hali ya wenye dhambi ina pande nyingi, lakini vyovyote unavyotaka kuitazama, Kristo amewaokoa watu wake kwa kifo chake cha upatanisho.
3
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
~ L. L. Morris. “Atonement.” New Dictionary of Theology. S. B. Ferguson, mh. (toleo tepe). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2000. uk. 55.
Jitahidi kuwasaidia wanafunzi kupitia mjadala huu kuona picha za kibiblia zenye pande nyingi na zenye mwingiliano wa kina kuhusu kazi ya Kristo msalabani, na kutafuta kutumia maana hizo katika hali na mazingira yao mahususi ya maisha.
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online