Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
1 2 6 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Kufikia mwisho wa kipindi kilichopita, ulipaswa kuwa umesisitiza kuhusu suala la wanafunzi wako kuwa wamefanya maandalizi ya msingi kwa ajili ya Kazi ya Huduma kwa Vitendo. Pia, kufikia wakati huu, wanafunzi wako wawe wamechagua kila mmoja kifungu cha Biblia kwa ajili ya Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko. Kazi zote mbili zitafanywa kwa ubora zaidi endapo wanafunzi wataanza kuzifikiria mapema zaidi na kuamua kile wanachotaka kufanya. Usikose kusisitiza hili, kwani, kama ilivyo katika masomo yoyote, mwishoni mwa kozi kunakuwa na mambo mengi yanayopaswa kukamilishwa, na wanafunzi wataanza kuhisi shinikizo la kudaiwa kazi kadhaa kwa wakati mmoja. Njia yoyote ambayo unaweza kutumia kuwakumbusha juu ya umuhimu wa kujipanga mapema itakuwa ya manufaa kwao, kwamba wanatambua hilo au la. Kwa sababu hii, tunashauri kwamba ufikirie kukata maksi kadhaa kwenye kazi zitakazokusanywa kwa kuchelewa. Hili halifanyiki kwa lengo la kuwaaibisha au kuwadhuru wanafunzi, bali kama fundisho la kuwafanya wafanye maandalizi ya kazi zao mapema, wasije wakalazimika kufanya kazi zao kwa shinikizo dakika za mwisho, na kujinyima fursa ya kufanya kwa ubora na kwa tafakuri ya kina katika mchakato wa kutekeleza kazi zote mbili. Ingawa kiwango cha maksi za kukatwa kinaweza kuwa cha kawaida, utekelezaji wako wa kanuni ulizojiwekea utawasaidia kujifunza kuwa makini, wenye ufanisi na kujali muda wakati wanapoendelea na masomo yao.
6 Ukurasa wa 244 Kazi
3
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online