Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 2 7

Mungu Roho Mtakatifu Nafsi ya Roho Mtakatifu

SOMO LA 4

Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi wa Somo la 4, Nafsi ya Roho Mtakatifu . Lengo la jumla la moduli ya Mungu Roho Mtakatifu ni kuwawezesha wanafunzi wako kuelewa Roho Mtakatifu ni nani (nafsi) na kile anachofanya (kazi), ili waweze kutetea ufahamu huu kwa kutumia Maandiko, na kuona matokeo ya kweli hizi katika huduma ndani ya Kanisa na kupitia Kanisa. Shabaha ya somo hili, kwanza, ni kuthibitisha kwamba Roho Mtakatifu ni Nafsi ya Kiungu; pili, kuelewa uhusiano wake na washirika wengine wa Utatu Mtakatifu; na tatu, kukiri kwamba Yeye ndiye Mpaji wa Uzima wa kiungu anayeumba, anayetegemeza, na kufanya upya maisha ya kimwili na ya kiroho. Madhumuni haya yameelezwa kwa uwazi katika malengo ya somo, na unapaswa kuyasisitiza katika somo lote, wakati wa majadiliano na katika muda wako wa kukaa na wanafunzi. Kadiri utakavyoweza kusisitiza malengo haya katika vipindi vyote darasani, ndivyo utakavyotoa nafasi nzuri zaidi kwa wanafunzi kuelewa na kufahamu ukubwa na uzito wa malengo haya. Usisite kuwashirikisha wanafunzi juu ya malengo haya kwa ufupi darasani kabla ya kuanza kipindi. Vuta usikivu wa wanafunzi kuelekea malengo haya, kwani, kiuhalisia, huu ndio moyo wa dhumuni lako la kielimu unapofundisha vipindi vya somo hili. Kila kitu kinachojadiliwa na kufanyika kinapaswa kulenga kwenye malengo haya. Tafuta njia za kuyasisitiza haya kila wakati, kuyakazia na kuyarudia tena na tena unapoendelea na somo. Msisitizo wa ibada hii ni ukweli kwamba mtu anayetaka kumjua Mungu anategemea huduma ya Roho Mtakatifu. Unapoanza somo hili la Roho Mtakatifu, bila shaka ni kweli kwamba una baadhi ya wanafunzi ambao wana ujasiri kuhusu uwezo wao wa kuelewa na kukamilisha kila kinachotolewa ili kujifunza na wengine wana wasiwasi . Kwa kawaida, mitazamo hii inatokana na historia ya mwanafunzi kielimu. Wanafunzi ambao wamefaulu katika taaluma hapo awali huwa na ujasiri wakati wanafunzi ambao wamepata shida au kushindwa huwa na wasiwasi. Kipindi hiki cha ibada kinakupa fursa ya kuzungumza juu ya hisia hizo. Ingawa kujifunza theolojia

 1 Ukurasa wa 245 Utangulizi wa Somo

4

 2 Ukurasa wa 245 Malengo ya Somo

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

 3 Ukurasa wa 245 Ibada

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online