Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
1 2 8 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
kunahusisha kusoma, kufanya kazi kwa bidii, na ujuzi wa kufikiri; si sawa kabisa na taaluma nyingine. Akili zetu haziwezi kumwelewa Mungu katika siri zake zisizo na kikomo na makusudi yake yasiyoweza kueleweka kikamilifu na wanadamu. Kuwa mwerevu au na uzoefu wa kielimu sio sababu ya kuwa na uhakika kwamba mtu atamwelewa Mungu kweli. Kinyume chake, sisi wanadamu tunapokuja kwenye elimu ya Mungu, sisi sote tunasimama kwenye uwanja sawa: Yeye yuko juu yetu kabisa! Kwa hivyo, ufahamu wowote wa kweli wa Mungu utakuja kupitia kazi ya neema ya Roho Mtakatifu. Wanafunzi wenye ujasiri wanapaswa kukiri kwa unyenyekevu kwamba uwezo wao wa kukariri taarifa au kucheza na dhana hautawafanya kuwa wanatheolojia. Wanamtegemea Roho pekee ili kuweza kupokea ufahamu wa kweli. Kwa upande mwingine, wanafunzi wenye hofu wanapaswa kuhakikishiwa kwamba ikiwa Mungu amewafanya viongozi katika Kanisa lake na amewaleta katika kozi hii kwa ajili ya mafunzo, Roho wake ana uwezo zaidi wa kuwapa hekima na ufahamu kwa kazi hiyo. Wao pia wanapaswa kumtegemea kabisa Roho wa Mungu. Kila mtu anayepokea mafunzo ya theolojia lazima aweke tumaini lake katika ahadi ya Kristo: Yn. 14:26 – Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. Unapotambulisha zoezi hili, tafadhali wahakikishie wanafunzi kwamba hutafuti kazi ya sanaa ya ubora wa juu! Wape wanafunzi dakika 2-3 za kufikiria wazo fulani na kulichora kwenye karatasi. Baada ya wanafunzi kumaliza kuchora, waalike kushirikisha michoro yao kwa kundi zima kama darasa ni dogo, au wagawanyike katika vikundi vidogo ili kushirikishana kama darasa ni kubwa. Kila mwanafunzi anaposhirikisha wengine anapaswa kueleza kwa nini alichagua kuchora kile alichokichora na jinsi kinavyo mwakilisha Roho Mtakatifu kwake. Kauli ya Mpito kuingia katika somo: “Mara nyingi watu hupata wakati mgumu kumwelewa Roho Mtakatifu na kuhusiana naye. Kwa kuwa ni jambo la kawaida katika maisha yetu kuwa karibu na akina baba na wana, tuna mahali pa kuanzia kuelewa maana
4
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
4 Ukurasa wa 246 Kujenda Daraja – Sehemu ya 1
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online