Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
1 3 0 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Mwana. Udhaifu wake ni kwamba unahusisha mtu mmoja kushika nafasi tatu. Mtu huyu hana vituo vitatu tofauti vya fahamu; yeye sio nafsi tatu. Bila maelezo sahihi, mfano huu unaweza kusababisha kufikiria Utatu kama uzushi wa ki-modali unavyofanya. Umodali ni uzushi unaokana Utatu kwa kufundisha kwamba Mungu ni mmoja ambaye, katika historia yote ya Biblia, amejifunua mwenyewe katika namna au hali tatu. Kulingana na Umodali , hakuna Nafsi tatu katika Uungu, lakini Nafsi moja anayecheza nafasi tatu tofauti. (Kumbuka: Uzushi wa Kimodali kwa kawaida hukanushwa kwa kutazama ubatizo wa Yesu ambapo Baba anazungumza na Roho anashuka wakati huo huo Yesu anapobatizwa, au kwa kutazama kusulubishwa kwake ambapo Yesu anahisi kuwa ameachwa na uwepo wa Baba. Katika matukio haya na mengine tunamuona Baba, Mwana, na Roho wakihusiana baina yao, jambo ambalo wasingeweza kufanya kama wangekuwa Nafsi moja katika majukumu tofauti). Waelekeze wanafunzi wafikirie na kujadili machache kuhusiana na vielelezo hivi na namna vinavyotusaidia au kufanyika vikwazo kwetu katika kufikiri kwa usahihi kumhusu Mungu. Kauli ya Mpito kuingia katika somo: “Somo letu la leo litatusaidia kugundua nafasi ya Roho Mtakatifu katika maisha ya Utatu. Tutajaribu kutafuta njia za kuelezea tofauti kati ya Mwana wa Mungu na Roho wa Mungu na tutajaribu kugundua njia ambazo Roho anahusiana na Baba na Mwana. Baadhi ya mawazo haya yatakuwa magumu kwa sababu tunazungumza juu ya fumbo kuu, lakini Kanisa limejifunza kutokana na uzoefu jinsi ilivyo muhimu kufikiria ipasavyo kuhusu asili ya Mungu na kusahihisha mawazo yasiyo sahihi kila yanapotokea. Haijalishi ni kwa kiwango gani mawazo hayo ya kitheolojia kuhusu Utatu yalivyo magumu, tunapaswa kukumbuka kwamba kweli za msingi zaidi za Utatu zaweza kupatikana kwa kukariri Kanuni ya Imani ya Nikea ambayo inaelezea kweli muhimu kuhusu asili ya Mungu katika aya chache tu.” Maandiko hayaonyeshi waziwazi kila mara endapo kinachoongelewa katika mstari fulani ni upepo, pumzi, roho ya mwanadamu, roho ambayo ni malaika au roho ambayo ni pepo mchafu au Roho wa Mungu. Ndio maana wakati fulani tunapolinganisha tafsiri kadhaa za Biblia utaona kwamba moja inatafsiri neno hilo kama pumzi na
4
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
7 Ukurasa wa 248 Muhtasari wa Kipengele cha II-B-1
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online