Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 3 1
nyingine inalitafsiri kama Roho. Aidha tafsiri moja inaweka herufi ya kwanza kuwa katika Herufi kubwa “Roho” kwa sababu inadhaniwa kwamba ni Roho wa Mungu anayezungumziwa hapo, wakati tafsiri nyingine haiweki herufi kubwa mwanzoni kwa kuwa inadhaniwa kuwa ni roho ya mwanadamu inayozungumziwa hapo. Linganisha Maandiko haya: • Zek. 12:10 Katika matoleo ya Maandiko ya Swahili Union Version na Swahili Roehl Bible SRB37 [Kama ilivyo katika matoleo ya Kiingereza ya King James Version na New King James Version] . Linganisha “roho ya neema na kuomba” na “Roho ya…..” • Ezekieli 37:9 Katika matoleo ya Maandiko ya English Standard Version , the New American Standard (NASB) , na the New English Bible (NEB) . Humo zingatia maana rejea za neno Roho: “pumzi,” “roho,” na “upepo.” Ezekieli 37:9 – Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapuzie hawa waliouawa, wapate kuishi. John Calvin anafuata nyayo za wanatheolojia wa kale wa Kanisa katika kuwatofautisha washirika wa Utatu kwa njia hii: Tofauti hii ni kwamba, Baba anahusishwa na mwanzo wa utendaji, chemchemi na chanzo cha vitu vyote; Mwana anahusishwa na hekima na shauri, na mpangilio katika utendaji, huku nguvu na ufanisi wa utendaji vikihusishwa na Roho [msisitizo ni wangu]. Wakati nafsi zote tatu kimsingi zinatenda katika umoja katika kila tendo linalotendwa na Mungu, tunaweza kumzungumzia Mungu Baba kuwa ndiye msingi wa kila tendo, Mungu Mwana (Logos) akiwa ndiye mpangiliaji wa kila tendo, na Mungu Roho ni mtekelezaji anayetimiliza kila tendo kwa nguvu. Hivyo mtazamo wa Agano la Kale juu ya Roho Mtakatifu kama nguvu ya Mungu katika utendaji unaendana kabisa na kazi ya Roho inayopatikana katika theolojia ya Agano Jipya ya Mungu katika Utatu. ~ Institutes , I.xiii.18.
4
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
8 Ukurasa wa 249 Muhtasari wa Kipengele cha II-B-2
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online