Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

1 3 2 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

KUMBUKA: Tunapozungumzia kazi za kila nafsi katika Utatu tunaongea kuhusu “fundisho la iktisadi ya Utatu” (yaani namna ambavyo Baba, Mwana na Roho wanafanya kazi kuhusiana na uumbaji wao) hii ikiwa kinyume na “fundisho la kiontolojia la Utatu” (yaani namna ambavyo Baba, Mwana, na Roho wanaendelea kuwepo—ikiwa na maana kwamba Baba mara zote anatoa [anazalisha], Mwana anatolewa, na Roho mara zote anatoka kwao). Umbo lililozoeleka zaidi la taswira ya hua katika Biblia linaonekana kwenye simulizi za ubatizo ambapo Roho wa Mungu anashuka kutoka mbinguni “kama hua” (Mt. 3:16)... Hata hivyo inambidi mtu afikirie kuhusu kitabu cha Mwanzo 1:2, ambapo Roho wa Mungu, maji, pamoja na mfano wa ndege vinaonekana tena (merahepet = “jongea” au “elea” ni taswira ya ndege, taz. Kumbukumbu la Torati 32:11). Katika Talmud (b. Hag. 15a) inafananisha kuelea kwa Roho juu ya maji wakati wa uumbaji na kupepea kwa njiwa, na pia 4!521, kipande cha Hati-kunjo ya Bahari ya Chumvi [Dead Sea Scroll], kinakipa kitabu cha Mwanzo 1:2 matumizi mengine ya kieskatolojia: Roho ataelea juu ya watakatifu katika siku za mwisho. Kwa hiyo njiwa wakati wa ubatizo anaonekana kuwa na maana kwamba Yesu analeta uumbaji mpya.

 9 Ukurasa wa 252 Muhtasari wa Kipengele cha III-B-2-d

4

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

~ Leland Ryken, James C. Wilhoit and Tremper Longman III, Gen. ed. “Dove.” Dictionary of Biblical Imagery. Downers Grove, IL/Leicester, England: InterVarsity Press, 1998. uk. 217.

Wasidie wanafunzi kuona kwamba huduma nzima ya Roho Mtakatifu ina dhumuni na kusudi lililokubwa zaidi la siku za mwisho. Kusudi la Mungu ni mbingu mpya na nchi mpya, inayokaliwa na jamii mpya ya wanadamu (Kanisa), na kuunganishwa katika amani kamilifu chini ya utawala wa Kristo. Roho sio tu anautegemeza ulimwengu wa sasa, lakini pia anafanya kazi kwa bidii ili kutimiza kusudi kuu la Mungu la uumbaji mpya.

 10 Ukurasa wa 254 Hitimisho

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online