Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 3 3

Zilizoorodheshwa hapa chini ni kweli za msingi zilizoandikwa katika mfumo wa sentesi ambazo wanafunzi wanatakiwa kuwa wamezipokea kutoka kwenye somo hili, ikimaanisha kutoka kwenye video walizotazama na mijadala waliyoifanya chini ya uongozi wako. Hakikisha kwamba dhana hizi zimefafanuliwa vizuri na zimewekewa mkazo kwa umakini mkubwa, kwasababu, kazi zao za majaribio na mitihani zitachukuliwa kutoka kwenye dhana hizo moja kwa moja. Katika kuwasaidia wanafunzi wako kufikiria hali zao wenyewe, unaweza kubuni baadhi ya maswali au kutumia yale yaliyotolewa hapa chini kama tu njia ya kuchochea shauku yao. Kilicho muhimu hapa sio maswali yaliyoandikwa hapa chini, lakini ni kwako wewe, katika mazungumzo na wanafunzi wako, kutatua kada ya masuala kadha wa kadha, mashaka, maswali, na mawazo ambayo yanatokana moja kwa moja na uzoefu wao, kisha husianisha hayo na maisha na huduma zao. Usisite kutumia muda mwingi kwa ajili swali fulani lililotokana na video, au jambo maalum ambalo linafaa hasa katika muktadha wa huduma wanazofanya wakati huu. Lengo la sehemu hii ni kuwawezesha kufikiri kwa kina na kitheolojia kuhusiana na maisha yao na mazingira ya huduma zao. Kwa mara nyingine, maswali yaliyopo hapa chini yametolewa kama miongozo na vichochezi tu, na hayapaswi kuonekana kama ya lazima. Chagua na uchukue kutoka katika hayo, au uje na maswali yako mwenyewe. Jambo la muhimu ni tija ya maswali hayo sasa, kwa muktadha wao na kwa maswali waliyo nayo. ya Kikristo. Lengo la mfano huu ni kuangalia na kuona kama wanafunzi wako wanaweza kutetea fundisho la Nafsi ya Roho Mtakatifu kwa maneno yao wenyewe kwa kutumia Maandiko. Hili ni muhimu kulifanya kwa sababu karibu kila kiongozi wa Kikristo atalazimika kufanya hivi wakati fulani katika huduma yake. Wanafunzi wanapopitia majibu yao, wakumbushe kwamba kuna mambo mawili ambayo kiongozi hasa wa kazi za kichungaji lazima ajibu. Kwanza, anapaswa kujibu yaliyomo katika nukuu au hoja iliyojengwa, anapaswa kusahihisha na kukanusha mafundisho Kushughulika na mafundisho ya uongo ya makundi ya Kikristo yenye imani potofu ni kipengele nyeti sana katika elimu ya theolojia

 11 Ukurasa wa 255 Muhtasari wa Dhana Muhimu

 12 Ukurasa wa 256

Kutendea kazi somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi

4

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

 13 Ukurasa wa 257 Mfano Halisi 1

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online