Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
1 3 4 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
ya uongo. Lakini pili, lazima pia kumjibu mtu aliyeleta hoja. Sue anapaswa kujibiwa kwa sauti gani? Je, yeye ni “mbwa-mwitu mkali” (Mdo 20:29; 2 Yoh. 10-11) anayejaribu kudhoofisha kundi kimakusudi? Au, yeye ni mtafutaji mpotovu na aliyechanganyikiwa anayehitaji mafundisho na matunzo ya kichungaji (2 Tim. 2:24-26)? Jambo muhimu zaidi kuhusu mfano huu ni kwa wanafunzi kutambua nguvu ya kauli ya Yesu katika Yohana 14:16 kwamba anamtuma Roho Mtakatifu kuwa “Msaidizi mwingine [paraclete].” Roho Mtakatifu daima anawakilisha na kutenda kwa uaminifu mahali pa Kristo kwa ajili yetu. Kama vile Yesu alivyoweza kudai kwamba mtu yeyote aliyekuwa amemwona yeye alikuwa amemwona Baba (Yohana 14:9), ni kweli vile vile kwamba mtu yeyote ambaye amemwona Yesu atamtambua Roho ambaye yeye amemtuma. Kukaa kwa Roho ndani yetu kunatuunganisha na Kristo Aliye Hai ili kwamba tuunganishwe katika upendo wake, nia yake, maneno yake, na matendo yake, kama matawi ya mzabibu. Tunamtambua Yesu na kumwitikia kwa imani kupitia kazi ya Roho Mtakatifu anaye tuangazia, na tunamtambua Roho na kumwitikia kwa sababu anamwakilisha Kristo na mafundisho yake kwa uaminifu. Katika kipindi hiki cha ufunguzi ni muhimu sana uanze kujenga uhusiano na wanafunzi wako. Waonyeshe kwamba unawajali kibinafsi na unajali wito wao wa huduma. Wao sio tu “wanafunzi” bali ni viongozi wa Kanisa. Wanapaswa kuona kwamba unaliona darasa hili, si tu kama ni kwa ajili ya mazoezi ya kitaaluma, bali kama njia ya kuwatayarisha ili kulijenga Kanisa na kutimiza makusudi ya Mungu. Wahimize wanafunzi darasani kuwashirikisha wengine hali halisi wanazokabiliana nazo katika huduma wiki hii na tumia muda kuwaombea na kutiana moyo. Hakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa zoezi la wiki ijayo, hasa lile la kuandisha muhtasari wa vitabu utakavyo waelekeza kusoma. Hili sio gumu; lengo ni kwamba wasome vitabu hivyo kwa kadiri wawezavyo na kuandika sentensi chache juu ya kile ambacho wanaamini waandishi walimaanisha. Huu ni ujuzi muhimu wa
14 Ukurasa wa 257 Mfano Halisi 2
4
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
15 Ukurasa wa 259 Ushauri na Maombi
16 Ukurasa wa 260 Kazi
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online