Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 4 1
Theolojia ya Kanisa Kanisa katika Ibada
SOMO LA 1
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi wa Somo la 1, Theolojia ya Kanisa: Kanisa katika Ibada . Lengo la somo hili ni kuwasaidia wanafunzi kuelewa Kanisa kama jumuiya ya watu ambao wamepata neema ya Mungu na ambao wanaitikia neema hii kwa kushiriki katika ibada kama wajibu na furaha yao. Somo litazingatia ukweli kwamba wokovu ni kwa neema kwa vile hapa ndipo mahali pa kuanzia kwa habari ya mwitikio wa ibada. Pia litazungumza kuhusu Meza ya Bwana na ubatizo kama njia mbili muhimu zaidi ambazo Kanisa hutambua, hupata uzoefu, na kuitikia neema ya Mungu. Kwa kuwa kuna tofauti halali kuhusu asili ya Meza ya Bwana na ubatizo miongoni mwa waumini wa madhehebu ya kiinjili, tafadhali uwe tayari kwa ajili ya kutokubaliana miongoni mwa wanafunzi wako kuhusu yale ambayo Biblia inafundisha. Kadhalika uwe tayari kuongoza mazungumzo ambayo ni ya haki na ambayo yatasaidia wanafunzi kustawisha imani zao katika mwanga wa Maandiko na theolojia ya madhehebu yao. Kwa kuwa lengo la somo hili ni ibada, hakikisha kwamba unadumisha “mioyo yenye uchangamfu” na pia “akili safi” kuhusu masuala haya. Wanafunzi wanapaswa kuongozwa katika shukrani na sifa hai wakati wa masomo haya pamoja na kutafakari juu ya masuala ya kitheolojia yanayohusika. Tafadhali soma kwa umakini malengo yafuatayo. Kadiri unavyoweza kuangazia malengo katika kipindi chote cha darasa, ndivyo unavyoongeza uwezekano wao wa kuelewa na kufahamu kweli muhimu ambazo ndio msingi wa somo hili. na Roho Mtakatifu. Mara nyingi tunaweza kufikiri kwamba ibada inahusisha aina fulani ya matendo ya kiibada, taratibu za sherehe za kidini, au utaratibu wa kiliturujia. Ibada ya Mungu haina mizizi katika jiografia au mafundisho ya kidini, bali, kama Yesu asemavyo, katika “roho na kweli” (Yn. 4:24). Baba hawezi kukaribiwa isipokuwa kwa njia ya Yesu Kristo (Yn. 14:6), ambaye dhabihu yake ya upatanisho imetuleta karibu na Mungu kwa imani (Ebr. 10:22-24). Kwa sababu Mungu ametujalia sisi kuingia katika uwepo wake, yaani, Patakatifu pa patakatifu kwa damu ya Yesu, na kwa sababu utukufu wa Mungu haulinganishwi na haubadiliki, Ibada hii inazingatia nia ya sifa na ibada zote zinazomwadhimisha Mungu: utukufu usio na kifani wa nafsi ya Mungu, Baba, Mwana,
1 Ukurasa wa 271 Utangulizi wa Somo
1
H U D U M A Y A K I K R I S T O
2 Ukurasa wa 271 Ibada
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online