Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

1 4 2 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

tunaendelea kuwa na sababu iliyo sahihi ya kumpa Mungu utukufu na heshima. Hatuhitaji kamwe kungoja hali ziwe nzuri na zenye kuvutia ajabu ili kumsifu Mungu; hata katikati ya janga la kutisha, hasara kubwa zaidi, uadui, na hitaji kuu zaidi, tunapaswa kutoa sifa na utukufu kwa Mungu. Licha ya yote tunayokabiliana nayo na yote tuanayoyajua, yeye ni Bwana wa yote, mkamilifu, mtukufu, mkuu, aliyejaa adhama na maajabu, ambaye hatatuacha wala kututupa kamwe. Bila kujali jinsi mambo yanavyoonekana, Mungu yuko na anabaki milele upande wetu na kwa ajili yetu. Kujifunza kutoa “dhabihu” ya sifa, tukibadilisha maana ya neno hili kwa muda, ni ujuzi mkuu ambao mwanafunzi wa Yesu anayekua anapaswa kuwa nao. Mara nyingi tutakabiliana na hali ambapo, kwa kuiangalia juu juu hali hiyo, hatuoni sababu hata moja ya kumsifu Mungu. Kila kitu kimekaa vibaya na giza; Mungu anaonekana kama hayupo, ama hajui, au hajali, au hawezi kusaidia. Katikati ya aina hii ya taabu, tushike vinubi vyetu na kumpa utukufu Yeye atupaye uhai na kutegemeza siku zetu. Anastahili kwa kuwa anastahili, kwa maana Jina lake ni “Niko Ambaye Niko.” Wape changamoto wanafunzi kuhusu wito wao wa kweli, sifa isiyoharibika na isiyo na kikomo kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya asili yake na kile ambacho amefanya katika Yesu Kristo. Mtunga Zaburi anathibitisha uwezo wa Neno la Mungu kufanya njia yetu kuwa safi (Zab. 119:9), kulinda dhidi ya nguvu za dhambi (Zab. 119:11), na kumpa uzima yeye anayelipokea (Zab. 119:93). Usigeuze muda wa kukariri Maandiko kuwa zoezi la kazi la darasani lililojawa na taratibu na marudio ya kuchosha. Tumia wakati huu kuwapa changamoto na kuwafundisha wanafunzi juu ya manufaa ya Neno lililokaririwa. Kariri Maandiko pamoja na wanafunzi, na upitie upya pamoja nao pale unapoweza. Jadili maana ya Maandiko, na jinsi yanavyohusiana kimaudhui na yale yaliyoshughulikiwa katika somo juma lililopita. Sehemu hii ya somo inaweza kuwa muhimu zaidi, kwa hivyo ichukue kwa umuhimu na heshima inayohitajika. Ni rahisi sana kulemewa na kulichukulia Neno lililokaririwa kama jambo rahisi la kutimiza kwa hitaji la somo. Kama mkufunzi, jaribu kulinda kipengele hiki dhidi ya kosa hili.

1

H U D U M A Y A K I K R I S T O

 3 Ukurasa wa 272 Mapitio ya Kukariri Maandiko

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online