Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 4 3

Acha wanafunzi wajadili kwa ufupi katika vikundi jinsi utambuzi huu ulivyotokea. (Hakuna wakati kwa kila mtu kutoa ushuhuda wake wote kwa hivyo hakikisha wanafunzi wanazingatia jambo maalum la wakati walipoelewa kuwa hawawezi kupata wokovu kwa jitihada zao). Warudishe wanafunzi pamoja na zungumza maneno haya: “Kanisa lipo kwa sababu ya neema ya Mungu pekee. Somo la leo linatusaidia kuelewa ibada kama mwitikio wa Kanisa kwa neema.” Sehemu hizi mbili za mwisho za Kujenga Daraja zinashughulikia mada inayofanana, yaani, tabia na ubora wa ibada yetu, na kile ambacho Mungu anataka au anakihitaji. Kilicho muhimu katika kuzingatia ibada hapa ni kanuni za kitamaduni na kijamii zinazohusiana na mazoea na matukio yanayochukuliwa kuwa ibada. Kwa maneno mengine, makanisa kwa kiasi kikubwa hayatambui kwamba ibada zao huwa zimeundwa kitamaduni na kihistoria, na kwamba ibada ya Mungu, kama madhihirisho ya ukweli na moyo, lazima iwe na sifa ya kuwa ya kina, ya kibinafsi, na ya moja kwa moja. Kamwe haitakuwa ibada kwa kupenda tu yale ambayo wengine wamefanya, tukitazamia hisia na shauku ambazo walikuwa nazo zitokezwe tena ndani yetu kwa kufanya tu matendo yao, kuimba nyimbo zao, au kuyaishi matendo yao. Ibada, kama madhihirisho ya Roho, kila mara itavikwa mavazi ya utamaduni lakini pia itatolewa kila wakati kwa Mungu aliye juu ya tamaduni zote, Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu. Kuwepo na kubadilika kwa mitindo na mbinu za kuabudu kunahusiana moja kwa moja na kuona kwamba Mungu ni Mungu wa wanadamu wote, na kwa hiyo anaweza kutukuzwa kihalali na kwa njia ya ajabu kupitia muundo wa kitamaduni wa dhati wa watu wowote ambao wametubu, wameamini, na wanamfuata na kumpenda Mwana wa Mungu, Yesu Kristo kwa Imani na tumaini. Moja ya makossa makubwa ambayo yamefanywa na makusanyiko mengi ya kiibada na Wakristo wengi ni kuamini kwamba baadhi ya maonyesho ya kitamaduni ya ibada ndiyo ibada yenyewe, yaani, njia ambayo ibada zote kila mahali zinapaswa kuzingatiwa na kufanyika. Kuruhusu uhuru wa kutoa shukrani zetu za kina na sifa kwa Mungu ni sehemu muhimu ya huduma ya kiongozi katika kuwaongoza wengine katika uwepo wa Mungu.

 4 Ukurasa wa 273 Kujenga Daraja – Sehemu ya 1

1

 5 Ukurasa wa 273 Kujenga Daraja – Sehemu ya 2 na ya 3

H U D U M A Y A K I K R I S T O

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online