Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
1 4 4 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Wanatheolojia mara nyingi hugawanya neema katika makundi ya maelezo. Neema ya kawaida inarejelea utunzaji wa Mungu juu ya watu wote ambao kwa huo anategemeza maisha (pumzi, mvua, chakula), anatoa ufahamu wa maadili, anatoa utawala wa kiraia, na kuzuia uovu ili kutoa fursa kwa maisha na utamaduni wa mwanadamu kustawi. Neema maalum inarejelea neema ambayo kwayo Mungu huwakomboa, kuwatakasa, na kuwatukuza watu wake. Neema tangulizi inarejelea neema ambayo huja kabla ya juhudi au maamuzi yoyote za kibinadamu na kufanya iwezekane kwa watu kutamani wokovu na kuitikia kwa imani. [Pelagius alifundisha kwamba] uwezo wa kutenda mema unakaa kiasili ndani ya hiari yenyewe, mbali na zawadi yoyote ya Mungu kwa asili ya mwanadamu, ili kwa kufuata kielelezo cha Kristo, njia ya wema ifunuliwe na watu kwa hiari zao wenyewe waweze kujiepusha na dhambi. Kwa hivyo hakuna haja ya utendaji wowote wa moja kwa moja wa Roho juu ya hiari ya mwanadamu ili kutenda mema, isipokuwa tu kwa Roho kufanya kazi kwa njia isiyo ya moja kwa moja kupitia dhamiri na akili. . . Kati ya mwaka 411 na 431B.K, si chini ya mabaraza ishirini na manne yalikabili suala la Upelagiani. Lilikuwa suala nyeti sana katika maisha ya ukomavu ya Augustine. . . . Mwitikio wa ukubalifu [wa Kanisa] uliboreshwa zaidi katika mabaraza la Efeso (431) na Orange (529), ambayo yalisimamia suala la ulazima wa neema katika matendo yote yanayohusiana na wokovu. “Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi hamuwezi, msipokaa ndani yangu.” (Yn. 15:4; rej. 1 Kor. 12:3).
6 Ukurasa wa 275 Muhtasari wa Kipengele cha I-C
1
H U D U M A Y A K I K R I S T O
7 Ukurasa wa 275 Muhtasari wa Kipengele cha I-D-1
~ Thomas C. Oden. The Transforming Power of Grace. Nashville: Abingdon Press, 1993. uk. 110-111.
Theolojia ya Kiinjili inaanza na dhana kwamba kanuni ya wokovu daima ni “kwa neema kwa njia ya imani.” Hakikisha kwamba kila mwanafunzi anaelewa ukweli huu wa msingi.
8 Ukurasa wa 276 Muhtasari wa Kipengele cha I-D-2
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online