Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 4 5
Ufafanuzi kuhusu Ibada Maneno makuu ya kibiblia, saha la Kiebrania na proskyneo la Kiyunani, yanasisitiza tendo la kusujudu.
9 Ukurasa wa 277 Muhtasari wa Kipengele cha II
~ E. F. Harrison, “Worship.” Evangelical Dictionary of Theology . uk. 1192.
Ibada ni kumwitikia Mungu kwa kutambua kikamilifu nafasi yake kama Anayestahili kabisa ibada, utii, utumishi, shukrani, na sifa. Zab. 95:6 – Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba (rej., Law. 26:1; Kum. 26:10; Zab. 138:2; Mt. 4:9 10). Baadhi ya Mawazo Muhimu Neno la msingi wa ibada: tunamwabudu Aliyefunuliwa kwetu. Kama si kusikia Neno la Mungu tusingeweza kumwabudu kwa sababu tusingemjua. Anakaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa. Tunaweza kumwitikia kwa sababu tu amejifunua. Yn. 1:18 – Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua Msingi wa kiagano wa ibada: tunaabudu kwa njia ya Kristo Yesu (Waebrania). Ibada ya Kikristo ni tofauti kwa kuwa ina msingi katika Kristo. Pazia limepasuliwa. Tuna njia ya moja kwa moja kwa Baba kupitia Kristo Yesu. Tukimtukuza Mungu Baba kupitia yeye. (Ebr. 10:20 BHN – Yeye ametufungulia njia mpya, njia ya uhai, kupitia lile pazia, yaani mwili wake mwenyewe…) Msingi wa kijumuiya wa ibada: ukuhani mtakatifu (ibada daima ni ya ushirika kwanza, ndiposa inakuwa ya mtu binafsi). Ebr. 10:25 – Wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.
1
H U D U M A Y A K I K R I S T O
Imekuwa ikisemwa kwamba sakramenti ni kama saini kwenye hundi. Hazilingani na pesa halisi katika benki au shauku ya mtu anayetia saini kukuona unapewa fedha, lakini zinafanya hayo yapate kuonekana. Saini yenyewe haitakuwa na thamani lakini hutumika
10 Ukurasa wa 277 Muhtasari wa Kipengele cha II-B
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online