Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
1 6 0 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
nao. Hakikisha kwamba dhana hizi zimefafanuliwa vizuri na zimewekewa mkazo kwa umakini mkubwa, kwa sababu, kazi zao za majaribio na mitihani zitachukuliwa kutoka kwenye dhana hizo moja kwa moja.
6 Ukurasa wa 333
Katika kuwasaidia wanafunzi wako kufikiria kupitia hali zao wenyewe, unaweza kubuni baadhi ya maswali au kutumia yale yaliyotolewa hapa chini ili kuchochea shauku zao. Ni muhimu uwasaidie wanafunzi kukuza mazoea ya kufikiri kwa kina, uwezo wa kutafakari sio tu kweli ni zipi lakini pia (na muhimu zaidi) nini maana ya kweli hizo katika mwanga wa maisha na huduma zao wenyewe. Kwa hiyo, tafadhali zichukulie sehemu hizi na maswali yake katika mwangaza sahihi. Kilicho muhimu hapa si tu kuuliza maswali yaliyoandikwa hapa chini, bali ni kwamba wewe, katika mazungumzo na wanafunzi wako, uweze kuwasaidia kutambua aina hiyo ya mambo, masuala, maswali, na mawazo yanayotokana moja kwa moja na uzoefu wa maisha yao. Usisite kutumia muda mwingi kwa ajili swali fulani lililotokana na video, au jambo maalum ambalo linafaa hasa katika muktadha wa huduma wanazofanya wakati huu. Lengo la sehemu hii ni kuwawezesha kufikiri kwa kina na kitheolojia kuhusiana na maisha yao na mazingira ya huduma zao. Kwa mara nyingine, maswali yaliyopo hapa chini yametolewa kama miongozo na vichochezi tu, na hayapaswi kuonekana kama ya lazima. Chagua na uchukue kutoka katika hayo, au uje na maswali yako mwenyewe. Jambo la muhimu ni tija ya maswali hayo sasa, kwa muktadha wao na kwa maswali waliyo nayo. Sehemu ya hali nzuri ya darasani ni pale ambapo wanafunzi wanaelewa vyema kuhusu majukumu yao ya darasani, yaani, wanajua kila kitu kuhusu kazi zao, maswali yao yote kuhusu kazi hizo yamejulikana na kujibiwa, na kwamba wewe kama mshauri au mkufunzi umejitayarisha kuwaongoza katika mada na somo linalofuata.
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi
3
H U D U M A Y A K I K R I S T O
7 Ukurasa wa 337 Kazi
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online