Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 5 9
Mk 9:37 – Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi; na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma. Lk 9:48 – akawaambia, Ye yote atakayempokea mtoto huyu kwa jina langu anipokea mimi; na ye yote atakayenipokea mimi ampokea yeye aliyenituma. Kwa kuwa aliye mdogo miongoni mwenu nyote huyo ndiye mkubwa Yn. 12:44 – Naye Yesu akapaza sauti, akasema, Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi bali yeye aliyenipeleka. Yn. 12:48 – Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho. Yn. 13:20 – Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeaye mtu ye yote nimpelekaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi; ampokea yeye aliyenipeleka. Maswali haya yameundwa ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaelewa malengo na kweli muhimu zilizowasilishwa kupitia video. Jukumu lako kama mkufunzi ni kutumia maswali haya kufanya mapitio ya dhana na maarifa muhimu yaliyowasilishwa kwa njia ya video, na pia kuwapima wanafunzi ili kuona ikiwa wameyaelewa kama yalivyowasilishwa. Bila shaka, itakuwa muhimu kwako kupima muda wako vizuri, hasa ikiwa wanafunzi wako wanavutiwa na dhana za somo, na wanataka kujadili matumizi yake kwa urefu. Kipindi chako cha darasa na urefu wake vinapaswa kukuongoza katika aina ya uhuru unaojipa wewe na wanafunzi wako katika kujadiliana masuala mbalimbali yanayotokana na uwasilishaji yako. Sehemu hii ya somo inakupa fursa ya kurejea dhana muhimu za somo zima na mawazo mengine yoyote ambayo yamejitokeza kupitia kujifunza kwenu pamoja mada husika. Kwa sababu hiyo, kauli zilizoorodheshwa hapa chini zinawakilisha kweli za msingi ambazo wanafunzi wanapaswa kuondoka nazo kutokana na maudhui ya somo hili, yaani, kutoka katika video na majadiliano yako pamoja
3
H U D U M A Y A K I K R I S T O
4 Ukurasa wa 331 Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu
5 Ukurasa wa 332 Muhtasari wa Dhana Muhimu
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online