Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
1 5 8 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Mit. 13:17 – Mjumbe mbaya huanguka maovuni; Bali mjumbe mwaminifu ni afya. Mal. 2:7 – Kwa maana yapasa midomo ya kuhani ihifadhi maarifa, tena yawapasa watu kuitafuta sheria kinywani mwake; kwa kuwa yeye ni mjumbe wa Bwana wa majeshi. Yn. 20:21 – Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. Lk. 10:16 – wasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma. Mdo. 26:17-18 – nikikuokoa na watu wako, na watu wa Mataifa, ambao nakutuma kwao; 18 uwafumbue macho yao, na kuwageuza waiache giza na kuielekea nuru, waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu; kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi. 2 Kor. 3:6 – Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha. Efe. 6:20 – ambayo kwa ajili yake mimi ni mjumbe katika minyororo; hata nipate ujasiri katika huyo kunena jinsi inipasavyo kunena. Kuwawezesha wanafunzi wako kuona kwamba wao, kwa hakika, wanamwakilisha Bwana Yesu aliyefufuka na kuinuliwa katika uongozi wao ni mojawapo ya vipengele muhimu vya kutia nguvu vya somo hili. Wanachojishughulisha nacho si juhudi nzuri tu au utunzaji; wanasimama mahali pa Bwana Yesu, kwa ajili ya utukufu wake, na yeye mwenyewe atawapa thawabu kwa sababu ya utii na uaminifu wao katika kutumikia mahitaji ya watu wake. Hii inalingana moja kwa moja na jinsi Bwana wetu alivyomtii Baba, na kwa hiyo Mungu alimwinua sana (Flp. 2:5-11). Vivyo hivyo, tunamheshimu Kristo, na hivyo atatuheshimu (Yn. 12:24-25). Hili lilitumika pia katika kupokea maneno ya mitume kama mafundisho ya Kristo mwenyewe (rej. 1 The. 4:8 – Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu). Angalia tena maana hii ya uwakilishi katika maandiko yafuatayo: Mt. 10:40 – Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma.
3
H U D U M A Y A K I K R I S T O
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online