Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 5 7

Usisite kujadili malengo haya kwa ufupi kabla ya kuingia katika kipindi. Vuta umakini wa wanafunzi kwenye malengo ya somo, kwani, katika maana halisi, hiki ndicho kiini cha lengo lako la kielimu kwa kila kipindi cha darasa katika somo hili. Kila kitu kinachojadiliwa na kufanyika kinapaswa kuwaelekeza kwenye malengo haya. Tafuta njia za kuyaangazia haya kila mara, ili kuyasisitiza na kuyakazia tena na tena kadri unavyoendelea. Katika uhalisia, kuzingatia malengo hukupa uwanja mpana wa kuvinjari mtiririko na maudhui ya darasa. Yarejee mara kwa mara pamoja na wanafunzi, na uhusishe mambo mbalimbali yanayo wavutia na mazungumzo unapowaongoza. Katika mambo yote, kanuni ya utendaji inapaswa kuwa kile ambacho Paulo alimwambia Timotheo: 2 Tim. 2:20-21 – Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina. 21Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema. Wanafunzi wote lazima wajitayarishe kwa kazi ambayo Bwana anaweza kuwaitia. Ni katika nia hii tunakuhimiza kuwahimiza wanafunzi wako kujitahidi katika ubora na kina. Ibada hii inazingatia dhana ya uwakilishi, ambayo ni lugha ya picha muhimu kwa uongozi wowote katika Maandiko, iliyofunuliwa na kuonyeshwa katika Agano la Kale na Agano Jipya. Maandiko kadhaa yanaangazia msisitizo huu; angalia namna kila moja linavyotoa hisia ya uwakilishi katika uongozi wa kiroho: 2 Kor. 5:20 – Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu. Ayu. 33:23 – Kwamba akiwapo malaika pamoja naye, Mkalimani, mmoja katika elfu, Ili kumwonyesha binadamu hayo yampasayo.

 2 Ukurasa wa 319 Malengo ya Somo

3

H U D U M A Y A K I K R I S T O

 3 Ukurasa wa 319 Ibada

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online