Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

1 5 6 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

Kikristo na episkopos linazingatia kazi ya viongozi wa Kikristo. Haya ni maelezo yanayoendana kabisa na maana ya maneno haya katika Maandiko. Kwa orodha kamili ya sifa za ofisi hizi rasmi tafadhali rejelea kwa umakini 1 Timotheo 3:1-7 na Tito 1:5-9. Watu wa hali ya juu zaidi kimaadili, kiroho, na kitheolojia ndio wanaostahili kuteuliwa katika nafasi za uongozi wa Kikristo katika Kanisa. Sababu ya sifa hizi njema iko wazi; wazee na maaskofu walipewa jukumu la kuongoza kundi la Bwana (Mdo. 20:28), kuwafundisha na kuwalea katika Neno la Mungu (1 Tim. 3:2), na kutoa uangalizi wa jumla katika mambo ya jumuiya, hasa kuwalinda dhidi ya makosa na mashambulizi ya watu wadanganyifu wasio waaminifu na udanganyifu wa adui (1 Tim. 5:17; Tit. 1:9). Ukweli kwamba mara nyingi wazee wanatajwa kuwa zaidi ya mmoja unadhihirisha kwamba ni lazima tuufikirie uongozi wa Kikristo kama wingi katika mwili wa Kristo; Mungu atainua idadi ya kutosha ya watenda kazi wa kiroho wenye sifa zifaazo ili kuwatunza watu wake (taz. Mdo. 14:23; Flp. 1:1; Tit. 1:5). Katika nafasi hizi mbili tunaweza pia kuongeza jukumu la mashemasi (Kiyu. diakonos ), au “watumishi” au “wahudumu” ambao majukumu yao yalionekana kulenga kutoa msaada kwa wazee, huku wakichukua jukumu la kuhudumia mahitaji ya mwili (taz. Mdo 6:1-6). Viongozi hawa walipaswa kuwa watu wa sifa njema na wenye kujitoa kwa Bwana (1 Tim. 3:8-13). Yote kwa yote, kupitia kwa wazee, maaskofu, na mashemasi, kwa neema ya Mungu Kanisa lake limekuwa likipata hazina ya ajabu ya watenda kazi wa kiroho ili kulinda, kulisha, na kutunza mwili wa Kristo. Katika sehemu ya malengo ya Kitabu cha Mwanafunzi utagundua kuwa malengo haya yameelezwa kwa uwazi, na unapaswa kuyasisitiza katika somo lote, wakati wa majadiliano na katika muda wako wa kukaa na wanafunzi. Kadiri utakavyoweza kusisitiza malengo haya katika vipindi vyote darasani, ndivyo utakavyotoa nafasi nzuri zaidi kwa wanafunzi kuelewa na kufahamu ukubwa na uzito wa malengo haya. Hakika, kadiri unavyofahamu zaidi malengo, ndivyo nyenzo za kufundishia zitakavyotosheleza na kuwa msaada zaidi kwa wanafunzi wako katika vipindi vyote.

3

H U D U M A Y A K I K R I S T O

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online