Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 5 5
Kutekeleza Uongozi wa Kikristo Uongozi Bora wa Ibada
SOMO LA 3
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi wa Somo la 3, Kutekeleza Uongozi wa Kikristo: Uongozi Bora wa Ibada – Ibada , Neno, na Sakramenti . Lengo la jumla la somo hili ni juu ya uongozi wa Kikristo, aina ya uongozi unaoweza kustawisha, kuandaa, na kuwawezesha wanafunzi mijini kwa ajili ya huduma. Somo hili linataka kuangazia njia ambazo viongozi wa Kikristo wanatoa huduma kwa usalama wa kiroho na ustawi wa wengine, wale ambao wanawaongoza katika namna rasmi au isiyo rasmi katika mwili wa Kristo. Mara moja, litakusaidia kuelewa, kuhakiki, na kuwafundisha wanafunzi wako muhtasari wa jumla wa kile kinachohusika katika uongozi wa Kikristo kama unavyoeleweka rasmi katika Agano Jipya. Kiujumla kuna majina mawili ya kiongozi katika Agano Jipya. La kwanza, “wasimamizi” au mzee (Kiyu. presbuteros ), ambalo hubeba maana ya mtu ambaye ni mzee na mwamini, ama kwa mwanamume mzee au mwanamke (1 Tim. 5:1, 2). Linatumika pia kwa viongozi wote wa Kanisa (Mdo. 14:23; 15:2, 4, 6) pamoja na wajumbe wa Sanhedrin (Matendo 4:5). Neno hili linazingatia hadhi, cheo, na kuaminiwa kwa ajili ya jukumu la uongozi wa Kikristo. Vivyo hivyo, linazungumza juu ya mamlaka na wajibu; wazee walikuwa na mamlaka ya kusimamia matumizi ya fedha za mwili wa Kristo kwa ajili ya ustawi wa wengine (Mdo. 11:30), kuamua masuala ya mafundisho na utendaji wa maadili (Mdo. 15:2-6, 22; 16:2), na kupokea taarifa kutoka kwa wainjilisti na mitume juu ya maendeleo ya kazi yao (Mdo. 20:17; 21:18). Walipaswa kukabidhiwa mamlaka, kuheshimiwa katika utumishi wao, na kutakiwa kufanya maombi kwa ajili ya wagonjwa na wale wanaohitaji huduma (1 Tim. 5:17; 1 Pet. 5:1-4; Yak. 5:14). Maana rasmi ya pili ya uongozi inahusiana na waangalizi, au maaskofu (Kiyu. episkopos ). Neno hili lilihusiana na wajibu wa kiongozi wa Kikristo kulinda au kusimamia kundi la Mungu, katika namna sawa na mchungaji anavyochunga kondoo wake. Vivyo hivyo, majukumu yote ya mchungaji yanahusishwa na jukumu la askofu, kulea, kulisha, kulinda na kutunza kundi la Mungu (taz. Mdo. 20:28; 1 Tim. 3:2; Tit. 1:7). Tunapolinganisha Maandiko ya Matendo 20:17, 28 na Tito 1.5,7, yaonyesha kwamba maneno “mzee” na “mwangalizi” yanatumiwa katika namna inayoonyesha kwamba yanarejelea cheo kilekile katika Kanisa. Baadhi wameeleza kwamba neno presbuteros linasisitiza heshima ya uongozi wa
1 Ukurasa wa 319 Utangulizi wa Somo
3
H U D U M A Y A K I K R I S T O
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online