Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

1 5 4 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

Sisitiza umuhimu wa unyenyekevu kwa wachungaji, kwa sababu kiuhalisia, kundi daima ni la Mungu na si la wale wanaolitumikia.

Kufikia mwisho wa kipindi cha pili, unapaswa kuwasisitiza wanafunzi umuhimu wa wao kuwa wamefanyia kazi ya awali na kufikiria kwa usahihi jinsi wanavyokusudia kutekeleza kazi yao ya Huduma kwa Vitendo. Pia, kufikia wakati huu, unapaswa kuwa umewasisitiza kuchagua kifungu watakachotumia kwa ajili ya Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko (yaani eksejesia). Kazi zote mbili zitafanywa kwa umakini na ubora zaidi ikiwa wanafunzi wataanza kuzifikiria mapema na kuamua kile wanachotaka kufanya. Usikose kusisitiza hili, kwani, kama ilivyo katika masomo yoyote, mwisho wa kozi mambo mengi hutarajiwa, na wanafunzi wataanza kuhisi shinikizo la kukamilisha kazi kadhaa kwa wakati mmoja. Njia yoyote ambayo unaweza kuwakumbusha juu ya hitaji la kupangilia mambo yao kwa umakini itakuwa ya manufaa kwao, iwe watalitambua hili mara moja au la. Kwa sababu hii, tunasisitiza kwamba uzingatie kukata maksi kadhaa kwa mitihani na kazi ambazo zitakusanywa kwa kuchelewa. Ingawa kiasi cha maksi utakazokata kinaweza kuwa kidogo, utekelezaji wako wa sheria utawasaidia kujifunza kuwa wafanisi na wenye kutunza muda wanapoendelea na masomo yao.

 4 Ukurasa wa 317 Kazi

2

H U D U M A Y A K I K R I S T O

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online