Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 5 3
walipokuwa wakipita chini ya fimbo mlangoni ili kujihakikishia kwamba hakuna aliyepotea. Wala kazi zake haziishi kwa machweo ya jua. Mara zote ilimbidi alinde zizi nyakati za giza kutokana na shambulio la wanyama wa mwituni, au majaribio ya hila ya mwizi anayevizia (ona 1 Sam. 17:34). ~ David M. Easton. Easton’s Bible Dictionary . (toleo tepe la chapisho la mwaka 1897). Oak Harbor, WA: Logos Research Systems, Inc., 1996. Kilicho muhimu kuelewa ni kwamba wito wa kuchunga ni wito wa kuwa kama Bwana Yesu, yule anayetoa mfano wa aina ya utunzaji wa kujidhabihu ambao lazima tuwe nao kwa wale walio wadogo. Wito huu wa uangalizi na ulinzi mkuu na wenye changamoto unatoa taswira kamili ya maana ya kuwatunza kondoo wa Bwana. Ni pale tu tunapoelewa ukubwa wa kazi hii ndipo tunaweza kufahamu aina ya mfano ambao Bwana wetu alijitengenezea, na aina ya changamoto inayohusika kwa wale tulioitwa kuwatunza watu wa Mungu. Ni dhahiri, kutokana na mijadala hii juu ya asili ya uongozi wa Kikristo, kwamba wanafunzi wako hawawezi kutarajia wengine kunyenyekea kwao isipokuwa tu ikiwa wao sasa hivi wananyenyekea kwa wengine . Hakuna njia yoyote ambayo mtu anapaswa kutarajia Mungu ampe mamlaka wakati anakataa kutii na kunyenyekea mamlaka halali ambayo Bwana amemweka chini yayo. Kanuni hii haiwezi kukiukwa na haibadiliki, na inatumika kwa wote katika uongozi au katika kuandaliwa kuwa kiongozi. Iwe mtu anatamani tu nafasi ya uongozi wa Kanisa au kwa sasa anayo nafasi ya mamlaka katika Kanisa, ni lazima aonyeshe unyenyekevu katika maisha yake mwenyewe ili kutarajia kunyenyekewa na wengine. Kwa hivyo, wanafunzi wako lazima waelewe umuhimu wa kuwapokea viongozi ambao Mungu amewapa kwa ajili yao (Efe. 4:7-11; 1 Pet. 5:1-5), kuwaheshimu katika kazi zote wanazofanya kwa niaba ya Kanisa (rej. 1 Tim. 5.17 “Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu, hasa wao wajitaabishao katika kuhubiri na kufundisha”). Hatimaye, wahimize wanafunzi wako juu ya umuhimu wa nidhamu ya utii kwa uongozi (Ebr. 13:7-9, 17, 24). Bila msingi huu thabiti wa heshima na utii, itakuwa vigumu kwao kuelewa jukumu la huduma ya kichungaji, au kuwa katika nafasi ya kuchunga wengine.
2
H U D U M A Y A K I K R I S T O
3 Ukurasa wa 316 Kuhusianisha Somo na Huduma
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online