Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
1 5 2 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Kama kawaida, umakini wako kwa malengo utakuwezesha kuwa makini na kuzingatia unapojadili asili ya pande nyingi za huduma ya kichungaji na wanafunzi wako.
Ibada hii inalenga hitaji letu la kufuata mfano wa Bwana wetu katika jukumu lake kama Mchungaji Mwema. Taswira ya mchungaji ni mojawapo ya lugha za picha zinazopendwa na muhimu sana katika kuonyesha aina ya utunzaji, malezi, na ulinzi unaohusika katika kuwaongoza watu wa Mungu. Katika uhalisia taswira hii, ingawa ni ya mashambani na si ya mijini, bado inatoa taswira yenye nguvu ya ajabu ya aina ya kujitoa ambako Mungu anatafuta kwa viongozi wake. Katika uhalisia, neno “mchungaji wa mifugo” linatumika sawa na neno “mchungaji wa kanisa” katika Maandiko ya Kiebrania (rej. Yer. 2:8; 3:15; 10:21; 12:10; 17:16). Mara nyingi taswira ya mchungaji hutumiwa kufananisha uhusiano wa Bwana na watu wa Israeli (Zab. 23:1; 80:1; Isa. 40:11; 44:28; Yer. 25:34, 35; Nah. 3:18). Dhana hii inachukuliwa na kupanuliwa katika namna Bwana wetu alivyokuwa akijielezea katika sura ya Mchungaji, na Mitume wanavyoitumia kumuelezea Bwana Yesu pia (Yn. 10:11, 14; Ebr. 13:20; 1 Pet. 2:25; 5:4). Taswira hii ya jukumu la kiongozi kulinganishwa na mchungaji ni ya kushangaza na ya wazi. Jukumu hili halikuwa rahisi wala la kustarehesha. Kuchunga kundi katika nchi yenye asili ya miamba kama Palestina ilikuwa ni suala hatari na gumu mno. Soma kwa umakini jinsi msomi mmoja anavyoelezea kwa muhtasari sura tofauti tofauti za kazi hii: Asubuhi na mapema aliliongoza kundi kutoka zizini, akiwaongoza mpaka mahali ambapo walipaswa kulishwa. Huku akiwaanglia mchana kutwa, alihakikisha kwamba hakuna kondoo yeyote aliyepotea, na akiwepo yeyote aliyepotea katika usimamizi wake kwa muda na kwenda mbali na wengine, anamtafuta kwa bidii mpaka ampate na kumrudisha. Katika nchi hizo kondoo huhitaji kunyweshwa maji kila mara, na kwa kusudi hilo mchungaji anapaswa kuwaongoza ama kwenye kijito fulani chenye maji au kwenye visima vilivyochimbwa nyikani na kuwekewa mabirika. Usiku alilirudisha kundi nyumbani katika zizi, akiwahesabu
2 Ukurasa wa 295 Ibada
2
H U D U M A Y A K I K R I S T O
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online