Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 5 1

Misingi ya Uongozi wa Kikristo Kiongozi wa Kikristo na Mchungaji – Poimenes

SOMO LA 2

Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi wa Somo la 2, Misingi ya Uongozi wa Kikristo: Kiongozi wa Kikristo kama Mchungaji – Poimenes . Lengo la jumla la somo hili ni jukumu muhimu ambalo taswira ya uchungaji inayo kwa uelewa wetu wa utendaji wa Uongozi wa Kikristo. Taswira hiyo ni muhimu kwa kila namna – Bwana wetu aliitumia mara nyingi kama taswira inayopendwa ya aina ya uhusiano alio nao na walio wake, na Mitume wakaichukua taswira hii ili kuelezea asili ya kazi ambayo viongozi wa Kikristo hufanya kuhusiana na Kanisa. Hata mtazamo wa haraka haraka sana wa taswira ya mchungaji katika Maandiko unaonyesha umuhimu wake kama lugha ya picha inayotujulisha maana ya Mungu ya uongozi na malezi ya Kikristo. A. D. Clarke anatupatia muhtasari mfupi wa baadhi ya picha muhimu zaidi za mchungaji katika Maandiko: Wachungaji wengi walichaguliwa kuwa viongozi muhimu wa watu wa Mungu, kwa mfano, Yusufu (Mwa. 37:2; 47:1-4), Musa (Kut. 3:1) na Daudi (1 Sam. 16:11; 17:15; Zab. 78:70-72). Mungu mwenyewe anatajwa tena na tena kuwa mchungaji wa watu wake (Mwa. 49:24; Zab. 23:1; 28:9; 80:1; Isa. 40:10-11; Eze. 34; Mik. 2:12; Mt. 25:32-33), na Yesu ndiye mchungaji mkuu wa kondoo (Yn. 10:1-18; Ebr. 13:20; 1 Pet. 2:25; 5:4; Ufu. 7:17; rej. pia Mt. 15:24). Wachungaji wabaya wanakemewa kwa kukosa kutunza kundi lao (Zek. 11:4-17), na Yeremia na Ezekieli wote wawili wanatumiwa na Mungu kuwakemea wale ambao wamekuwa wachungaji wabaya juu ya watu wake. Mungu mwenyewe atalikusanya kundi tena ndani ya zizi na ataweka wachungaji wapya watakaolitunza (Yer. 23:1-4; Eze. 34:23-24). Anawaita viongozi wawe wachungaji (2 Sam. 5:2; 7:7), na jukumu la kiongozi mcha Mungu ni kuwasimamia, kuwatunza, kuwalisha na kuwalinda kondoo (Yer. 3:15; Yn. 21:15-17; Mdo. 20:28; 1) Pet. 5.1-3). Hakuna lugha bora zaidi ya kuelezea umuhimu wa taswira hii, na kwa hiyo changamoto yako itakuwa kuwasaidia wanafunzi wako kupata ufahamu thabiti wa vipengele vyake na matokeo yake kwa uongozi wa Kikristo. Kuwa kiongozi wa Kikristo ni kuchunga, kuwa mchungaji wa kundi la Mungu au, kama Clark anavyosema, “kusimamia, kutunza, kulisha, na kulinda kondoo.” Katika somo hili lote tutachunguza taswira hii, na kupima umuhimu na matokeo yake kwetu leo tunapotafuta kuwaongoza watu wa Mungu katika utimilifu wake. ~ A. D. Clark. “Leadership.” New Dictionary of Biblical Theology . (toleo tepe). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2001.

 1 Ukurasa wa 295 Utangulizi wa Somo

2

H U D U M A Y A K I K R I S T O

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online