Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

1 5 0 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

Kanisa leo. Kila moja ya mifano ifuatayo inaweza kueleweka kupitia safu ya mitazamo na kanuni zilizofundishwa katika somo hili. Lengo, bila shaka, si kutoa jibu kamili ili kufafanua hali fulani au kutatua tatizo fulani, bali ni kuwasaidia wanafunzi kupata ujuzi katika kushughulikia matatizo na masuala fulani yaliyopo, huku wakizingatia kanuni mahususi za kibiblia. Wakiwa wamejihami na kweli ya Neno na uzoefu wa historia na mapokeo ya Kikristo, wanafunzi wanaweza kutumia uzoefu wao na ufahamu wao wenyewe kusaidia kutengeneza mielekeo mipya ya uelewa na kushughulikia maswali haya. Wasaidie kutumia kanuni tofauti kwa hali tofauti na kuona jinsi kanuni hizo zinavyoweka wazi maswali ya msingi au masuala ambayo yanahitaji kushughulikiwa. Mara zote watie moyo wanafunzi wasisome tu neno la Mungu, wakifurahia shughuli zao muhimu, lakini pia kuomba kwa bidii juu ya masuala, na hivyo kutumia karama na uwezo wao wa kiroho. Masuala yote tunayokabiliana nayo kama viongozi yatahitaji maombezi yetu maalum na endelevu, na kwa kusisitiza hili katika masomo yetu tunawazoeza wanafunzi wetu wasijifunze kamwe Biblia bila kurejelea hekima ambayo ni Mungu pekee anayeweza kutoa, aina ya hekima ambayo haitatuaibisha kamwe lakini itatuwezesha kumwakilisha Mungu kama apendavyo (Yak. 1:5-8). Kukiri kwamba hatuelewi kitu kamwe si tatizo kwa Bwana; Mungu yuko juu yetu na atatupatia hekima ikiwa tutaitafuta kwa mioyo yetu yote, na si kwa akili zetu zote pekee (Mit. 2:1-9). Kama vile mwandishi wa Mithali anavyodokeza, hatupaswi kamwe kutegemea fahamu zetu kana kwamba tunaweza kupata majibu kwa sababu tulifikiri vyema (Mit. 3:5-6). Wazoeze wanafunzi, hata baada ya kuligeukia Neno kwa mashauri, wamtazame Mungu katika maombi. Sio maombi au Neno, lakini ni maombi pamoja na Neno ndivyo vilivyoipamba huduma ya mitume, na vinapaswa kuwa tabia yetu (Mdo 6:4). Wahimize wanafunzi wako kutafuta uso wa Bwana katika maombi na kumwomba maarifa, mbinu, na suluhu maalum kwa masuala na mambo yenye mashaka wanayokabiliana nayo, katika maisha yao ya kibinafsi na pia huduma zao.

1

H U D U M A Y A K I K R I S T O

 23 Ukurasa wa 292 Ushauri na Maombi

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online