Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 4 9
na wanafunzi wako, na uangalie mambo yoyote ambayo yanaweza kukutoa kutoka kwenye msisitizo wa kweli muhimu na mambo makuu ya somo.
Hakikisha kwamba unatofautisha kati ya mwitikio wa Kanisa katika ibada yake kwa Mungu (ibada kulingana na matokeo yake) na uzuri wa Bwana, tabia yake na kazi yake katika Yesu Kristo (ibada kulingana na sababu yake). Kwa bahati mbaya, baadhi ya mijadala ya ibada imejikita zaidi kwenye namna tunavyoabudu badala ya sababu zinazotufanya tuabudu . Ingawa yote mawili ni muhimu katika kuelewa wito wa Kanisa kama ukuhani wa kiibada wa waamini, ni muhimu kwamba lengo libaki kwa Mungu ambaye tunamwabudu, na sababu ya wazi kwa nini sisi ni jumuiya ya kiibada. Ni pale tu dhana hizi zinaporejelewa na kuwekwa wazi ndipo tunaweza kufikiria kiusahihi njia tunazopaswa kumkaribia Mungu. Sababu ya ibada lazima itangulie dhana ya “ nini” na “ namna gani” ya kuabudu. Kauli hii haipaswi kueleweka kama rufaa ya kudharau umuhimu wa majadiliano juu ya mwitikio wa wanadamu kwa Mungu. Hata hivyo, ni kusisitiza kwamba umuhimu wa ibada unatokana na kuelewa kwamba Mungu anastahili kusujudiwa na kupewa utii wetu. Majadiliano ya ibada yanapaswa kuanza na kumalizika katika msingi wa Mungu na sio msingi wa wanadamu. Ingawa kuna matokeo mengi binafsi kwa fundisho hili la ibada, itakuwa muhimu kwako kama mkufunzi kuwasaidia wanafunzi kutunza asili ya ushirika katika maswali na masuala yote. Tabia ya kugeuza mjadala kuhusu Kanisa katika Ibada kuwa “mimi katika ibada” imeenea sana, na uwezo wako, katika mapitio na kutafakari na wanafunzi, ili kuwafanya wabaki kwenye matokeo ya kijumuiya ni muhimu hapa. Mifano hii halisi inaangazia masuala yahusuyo asili ya ibada katika makusanyiko yetu. Hitaji hapa ni kuwawezesha wanafunzi wako kuelewa mafundisho ya jumla, kweli, na kanuni zinazohusiana na Kanisa katika Ibada, na uwezo wao wa kutumia kanuni hizi katika changamoto za maisha halisi yanayohusiana na ibada ya
20 Ukurasa wa 287 Muhtasari wa Dhana Muhimu
1
H U D U M A Y A K I K R I S T O
21 Ukurasa wa 288
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi
22 Ukurasa wa 289 Mifano Halisi
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online