Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 6 3

Huduma ya Kuwakamilisha Watakatifu Huduma ya Mahubiri – Kerygma

SOMO LA 4 4

Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi wa Somo la 4, Huduma ya Kukamilisha Watakatifu : Huduma ya Mahubiri – Kerygma . Lengo la jumla la somo hili ni kuangazia nafasi ya Roho Mtakatifu na mbinu katika kuhubiri kwa ufanisi kibiblia. Kwa mtazamo wa haraka, inaweza kuonekana kwamba utegemezi kwa Roho Mtakatifu na mbinu ya uwasilishaji ni vitu visivyotegemeana; Je, kumtegemea Roho si kivuli cha kutozitegemea mbinu za kibinadamu? Ingawa itajadiliwa kote katika somo hili kwamba Roho pekee ndiye anayeweza kuwawezesha wanaume na wanawake kuielewa kweli ya Neno la Mungu na kuitumia maishani mwao, pia tutatetea busara, bidii, na nidhamu katika maandalizi ya ujumbe na ufahamu wa kanuni nzuri za mawasiliano katika uwasilishaji wa jumbe za mahubiri. Katika uwasilishaji wowote wa Neno la Mungu, unyofu hautoshi. Tunaunga mkono himizo la Paulo kwamba, chochote ambacho Bwana amekupa (pamoja na karama za Neno za kuhubiri na kufundisha), fanya kwa nguvu zako zote na kwa hali ya ubora na kwa nidhamu (rej. Rum. 12:4-8). Katika somo hili tunaangazia tena jukumu la upako wa kiungu na kutiwa nguvu katika utoaji na upokeaji wa ujumbe wa Neno la Mungu. Hapa, kwa mara nyingine tena, itakusaidia kusoma muhtasari uliopangwa vizuri wa umuhimu wa theolojia ya kuhubiri kwa maendeleo ya uongozi wa Kikristo, na K. Runia anatupatia muhtasari kama huu: Katika Biblia, kuhubiri kuna sehemu kubwa. Hili ni kweli kwa Agano la Kale (rej. Unabii), lakini hasa katika Agano Jipya. Mtu anaweza hata kusema kwamba Agano Jipya lenyewe ni matokeo ya mahubiri. Injili na nyaraka zote ni zao la kerygma . Yesu mwenyewe aliendelea kutangaza kuja kwa ufalme wa Mungu. Hata zaidi, katika shughuli zake za kuhubiri na kuponya ufalme ulikuwa tayari upo. Katika msalaba na ufufuo wake tendo la Mungu la ukombozi wa kieskatolojia lilifanyika. Hii ndiyo sababu pia baada ya kufufuka kwake na kumwagwa kwa Roho Yesu mwenyewe ndiye ujumbe mkuu wa mahubiri ya kitume. Kwa hiyo haishangazi kuona kwamba Agano Jipya linatumia zaidi ya vitenzi thelathini kuashiria shughuli ya kuhubiri. Mitume, walioagizwa na Bwana aliyefufuka, walihubiri ujumbe huu kama neno lenyewe la Mungu (taz. 2 Thes. 2:13). Nyaraka za Paulo mara nyingi zimetumia maneno kama vile ‘neno la Mungu’ au ‘neno la Bwana’ au, kwa njia fupi zaidi, ‘neno’ (rej. 1 The. 1:6, 8; 3:1; Kol. 4:3; 2 Tim. 2:9; Katika vifungu hivi vyote maneno hayo

 1 Ukurasa wa 339 Utangulizi wa Somo

4

H U D U M A Y A K I K R I S T O

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online