Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
1 6 4 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
yanarejelea neno lililohubiriwa (taz. TDNT IV, 116). Hii ndiyo sababu pia iliyopelekea neno lililohubiriwa na Paulo na wengine likawa lenye ufanisi. Ufanisi huu hautokani na kipaji cha mhubiri, lakini siri iko katika umiliki: ni neno la Mungu au la Bwana. Katika jumbe za kitume (mara zote msisitizo uwapo kwenye maudhui) sauti ya Mungu aliye hai inasikika. Msisitizo huu ulitolewa na Wanamatengenezo. Luther na Calvin wote waliamini kwamba, wakati ujumbe wa Injili ya Yesu Kristo unatangazwa, Mungu mwenyewe anasikilizwa na wasikilizaji. Katika sura ya 1 ya Maungamo ya Pili ya Helvetic (1566) Heinrich Bullinger, mrithi wa Zwingli, alitoa muhtasari wa msimamo wa Wanamatengenezo kwa kauli moja fupi: Praedickatioverbi Dei est verbum Dei – kuhubiriwa kwa neno la Mungu ni neno la Mungu. Katika sentensi ifuatayo anafasiri usemi huu kama ifuatavyo: ‘Kwa hiyo neno hili la Mungu (=Maandiko) linapohubiriwa sasa katika Kanisa na wahubiri walioitwa kihalali, tunaamini kwamba neno lenyewe la Mungu linatangazwa na kupokelewa na waamini.’ Sharti la lazima kwa mahubiri ya kweli ni kutangazwa kwa uaminifu kwa ujumbe wa Maandiko. Hata hivyo kuhubiri si marudio ya kawaida tu ya ujumbe huu. Ni lazima pia yafanywe kuwa halisi katika hali ya sasa. Ili mahubiri yaweze kuwa ya kweli na yenye kuufaa wakati husika, ujumbe wa Maandiko lazima uelekezwe kwa watu katika hali yao halisi ya kihistoria. Huenda ujumbe wa kibiblia usikubaliane na hali ya leo, lakini ni lazima ‘ukubaliwe’ (Calvin) katika muktadha huo. Kama vile katika Kristo Mungu alivyoshuka ili kuchukua mwili wetu (taz. Maafikiano, Umwilisho), vivyo hivyo katika kuhubiri neno Roho Mtakatifu hushuka ili kuwafikia watu katika hali zao. Kwa hiyo mhubiri lazima awe mfafanuzi wa Maandiko na wa kusanyiko lake, ili neno lililo hai la Mungu kwa ajili ya leo lisikike katika muunganiko wa andiko na hali halisi. ~ K. Runia. “Theology of Preaching.” The New Dictionary of Theology . S. B. Ferguson, mh. (toleo tepe). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2000. uk. 527-28. Lengo lako katika somo hili ni kuwashawishi wanafunzi juu ya ulazima kamili wa kunyenyekea chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu katika utangazaji wote wa Neno, pamoja na matumizi yenye nidhamu na bidii ya kanuni nzuri za mawasiliano, haswa wanaposhughulika na tamaduni na hadhira za mijini. Tutasisitiza kote katika somo hili umuhimu wa utamaduni katika mawasiliano yote ya kibiblia yenye
4
H U D U M A Y A K I K R I S T O
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online