Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 6 5
ufanisi, na unapaswa kufanya kama Runia asemavyo, na kuwasaidia wanafunzi kuwa wafafanuzi wa Maandiko pamoja na wasikilizaji wao ili Neno la Mungu liweze kutumika kwenye maisha yao kwa nguvu na ustadi kadiri iwezekanavyo. Tazama tena malengo ya kujifunza yaliyoorodheshwa katika somo, na kama kawaida, wajibu wako kama Mshauri ni kusisitiza dhana hizi katika somo lote, hasa wakati wa majadiliano na muda wote uwapo na wanafunzi wako. Kadiri unavyoweza kuangazia malengo katika kipindi chote cha darasa, ndivyo uwezekano kwamba wataelewa na kufahamu ukubwa wa malengo haya unavyoongezeka. Ibada hii inakazia hitaji la sisi kujitayarisha kwa ajili ya utoaji wa Neno la Mungu kwa wengine, yaani, kufahamu mambo yote yanayohusika katika uwasilishaji wa Neno la Kristo kwa waliopotea. Paulo katika 2 Wakorintho 4 anaweka wazi kwamba shetani ni mhusika mwenye bidii katika tukio la kuhubiri, akitumia muda kutafuta kuwapofusha na kuwadanganya wasikilizaji kuhusiana na kweli ya Kristo na uwezo wake wa kuokoa na kubadilisha maisha yao. Hata hivyo, Paulo ana uhakika kwamba uweza wa Bwana Yesu unaweza kushinda mbinu hii ya udanganyifu na upofu, na anadokeza kwamba utukufu uleule wa Mungu unang’aa kwa uangavu katika uso wa Yesu Kristo, Yesu yule yule ambaye ndiye ujumbe wa mahubiri yake ya Injili. Kwa namna nyingi, uwasilishaji wa Injili unaweza kueleweka kwa njia rahisi kimsingi. P. J. H. Adam anatoa muhtasari wa urahisi na uwasilishaji huu katika makala ya theolojia ya kuhubiri: Tunaweza kufupisha theolojia ya kibiblia ya kuhubiri kwa maneno haya: Mungu amesema, Imeandikwa, na Lihubiri neno (P. Adam, Speaking God’s Words , uk. 15-56). Mungu amesema. Ufunuo binafsi wa Mungu daima huonyeshwa au kuelezewa kupitia maneno. Ni kupitia maneno ambayo Mungu amesema tunamjua Yeye ni nani, kwamba ameumba ulimwengu, na maana ya kazi zake, na matendo yake ya kuokoa. Ni kwa maneno haya ndipo tunajua utambulisho na umuhimu wa Mwana wake Yesu, mpango wake wa wokovu, na wa Injili. Ni kwa maneno haya ndipo tunajua namna tunavyopaswa kuitikia neema ya Mungu kwa utiifu wa imani, na kutazamia kurudi kwa Kristo na utimilifu wa Ufalme wa Mungu.
2 Ukurasa wa 339 Ibada
4
H U D U M A Y A K I K R I S T O
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online