Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
1 6 6 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Mungu amejiweka katika namna yetu na kujinyenyekeza kunena kwa lugha ya kibinadamu, kwa maneno ya kweli kabisa, ili tuweze kumwitikia kwa imani tunaposikia sauti yake. Mungu anapokuwapo, yupo kuzungumza. Ingawa kuna wakati alizungumzia duniani, sasa anatuonya kutokea mbinguni (Ebr. 12:25). Wazo la ufunuo wa Mungu kama “kuzungumza” au “maneno” lina nguvu sana kiasi kwamba linatumika kama lugha ya picha kwa ufunuo wa Mungu katika Mwana wake. Kwa hiyo katika Waebrania 1 tunasoma kwamba “Mungu ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii . . . kwa sehemu nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana.” Paulo anaandika juu ya Yesu kwamba “alihubiri amani”; na Yohana anamfafanua Yesu kuwa “Neno” (Ebr. 1:1-2; Efe. 2:17; Yoh. 1:1). Mungu hutumia maneno kufunua Neno. Imeandikwa. Mungu anapokuwa amezungumza wakati mwingine hufanya maneno yaandikwe kwa ajili ya vizazi vijavyo. Katika Biblia nzima tunamwona akifanya hivi. Musa haongei tu na watu wa Israeli maneno ambayo Mungu amesema, bali pia anayaandika, ili vizazi vya baadaye, ambavyo vimefanywa kuwa watu wa Mungu kwa matendo yale yale ya kuokoa, waweze kujua kwamba yuko katika uhusiano wa agano pamoja nao. Mahubiri ya Musa kwenye uwanda wa Moabu yameandikwa, si kwa ajili ya wasikilizaji wa wakati huo tu, bali pia kwa vizazi vijavyo vya watu wa Mungu. Maandiko hayo ya kale yanapogunduliwa tena, kusomwa, na kupewa utii, kama katika nyakati za Yosia na Ezra, kuna uamsho. Maneno ya Mungu pia yaliandikwa kwa ajili yetu “ambao mwisho wa nyakati umetufikia” (1 Kor. 10:11 SNT). Tunapokuwa sehemu ya watu wa Mungu tunarithi ahadi hizi, maagano, na maonyo haya. Katika nyakati za Agano Jipya, baadhi ya mafundisho ya Yesu na wafuasi wake yaliandikwa kwa manufaa si tu ya wasomaji wa awali bali pia vizazi vilivyofuata vya watu wa Mungu. Maneno haya yote yamehifadhiwa, au yameandikwa, kwa ajili ya watu wa Mungu wanaoishi katika siku za mwisho, ambazo zilianza na ujio wa kwanza wa Yesu na zitaisha kwa kurudi kwake. Kama vile matendo ya Mungu ya kuokoa yalivyokamili, ndivyo pia ulivyo ufunuo wa maneno unaoyafafanua.
4
H U D U M A Y A K I K R I S T O
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online