Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 6 7

Hubiri neno. Wito wa kuhubiri neno unasikika katika Biblia nzima kwa njia nyingi tofauti. Ibrahimu kama nabii anapaswa kuwafundisha watu wa nyumbani mwake, na Musa nabii anapaswa kusema, kuandika na kusoma maneno ya Mungu kwa ajili ya watu wa Mungu. Makuhani wa agano la kale wana wajibu wa kufundisha sheria iliyotolewa kupitia Musa, na manabii kutumia sheria kwa kizazi chao wenyewe. Wanaume na wanawake wenye hekima hufundisha wengine njia ya hekima; wanafunzi wa Kristo wanahubiri Ufalme wa Mungu; mitume, wachungaji na waalimu huisema kweli ili kuwaleta watu kwenye imani katika Kristo, na kuwafanya wakomavu katika Kristo. Hitaji kubwa katika kanisa la baada ya mitume ni waalimu, wanaoweza kufundisha kweli na kukanusha makosa. Waumini wa kawaida wana wajibu wa kutiana moyo kwa maneno ya Mungu (1 The. 4:18); wanapofanya hivyo “neno la Kristo” linakaa kwa wingi ndani yao (Kol. 3:16) na kutiana moyo huku ni dawa ya Mungu kwa udanganyifu wa dhambi (Ebr. 3:13). Kwa hiyo haishangazi kwamba Paulo anamwagiza Timotheo kuhubiri neno (2 Tim. 4:2).

4

~ P. J. H. Adam. “Preaching and Biblical Theology.” The New Dictionary of Biblical Theology . T. D. Alexander, mh. (toleo tepe). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2001.

Waalike wanafunzi wako katika uthubutu kwa fursa hii ya ajabu na wajibu mzito walio nao wa kuhubiri kwa uwazi, ujasiri, na bila kugoshi Neno la Mungu aliye hai. Hii ni kazi yao, fursa yao, na wajibu wao usioyumbishwa.

H U D U M A Y A K I K R I S T O

Usichukulie kuwa ni jambo la kawaida sana au lisilo la lazima kuwauliza wanafunzi kama wanahitaji maombi kwa ajili ya mtu fulani au kitu kinachohusiana na mawazo na kweli zinazofundishwa katika somo. Maombi ni njia ya ajabu ya kutumia kweli kwa njia ya vitendo na yenye manufaa; kupitia kupeleka mahitaji maalum kwa Mungu kwa kuzingatia ile Kweli ya Neno la Mungu, wanafunzi wanaweza kuimarisha mawazo hayo katika nafsi zao, na kupokea tena kutoka kwa Bwana majibu wanayohitaji ili kutegemezwa katikati ya huduma zao.

 3 Ukurasa wa 361 Ushauri na Maombi

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online