Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 7 1
Misingi ya Utume wa Kikristo Maono na Msingi wa Kibiblia wa Utume wa Kikristo
SOMO LA 1
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi wa Somo la 1, Misingi ya Utume wa Kikristo: Maono na Msingi wa Kibiblia wa Utume wa Kikristo . Lengo la jumla la somo hili litakuwa kufuatilia wazo la hadithi ya mapenzi ya kiungu na vita vya milki kama mada kuu mbili za Maandiko ambazo zinatoa maana kamili na muhimu kwa uelewa wetu kuhusu utume. Dhana ya jumla ya somo hili ni kwamba umisheni hauwezi kamwe kupunguzwa kuwa aina ya uinjilisti, mbinu ya huduma ya mjini, au seti ya huduma ili kukidhi mahitaji ya wengine. Umisheni unajumuisha aina hizi na nyinginezo za ushuhuda na matendo mema, lakini kimsingi umisheni ni muendelezo wa tamthilia ya kiungu, mapenzi, vita na ahadi. Tunasisitiza kwamba misiolojia ya kweli huanza na hadithi ya Maandiko juu ya Mungu na watu wake, Mungu na uumbaji wake, na kutokea mahali hapa salama, kisha huanza kuunda, kuathiri, na kuongoza shughuli na mzigo wetu wa umisheni. Umisheni unaoanza na juhudi za kibinadamu si wa kibiblia, kwa namna yoyote. Ili utume uweze kuvuviwa na Bwana ni lazima uanze na kusudi la Bwana, moyo wake, na kazi yake, tendo hilo la ukombozi linalofikia kilele katika nafsi na huduma ya Yesu wa Nazareti. Chochote kilichopungufu la haya sio umisheni hata kidogo. Katika uhalisia, kuelewa umisheni (au nyanja nyingine yoyote kuu ya theolojia na misiolojia) ni kujifunza matumizi ya waandishi waliovuviwa ya taswira, lugha ya picha, ishara, na hadithi. Kupitia matumizi yaliyovuviwa ya mawazo, waandishi wa Biblia wametujulisha mpango na kusudi la Mungu. Uwezo wetu wa kufuata mawazo na mantiki yao hautawezekana ikiwa tutapuuza uwezo wa matumizi ya mawazo ya Kikristo (na ufahamu wa kibiblia). C. Seerveld anaweka wazi jambo hili: Dhana ya Kikristo ya mawazo itatofautisha kuwaza kunakotokana na makosa katika utambuzi, dhidi ya kujenga taswira na dhidi ya na utabiri wa ukweli. Shughuli ya kimawazo ya binadamu ni tofauti kabisa na hisia au kufikiri lakini pia ni shughuli halali inayohusiana na utendaji kazi wote wa binadamu. Kufikiri ni zawadi ya Mungu ambayo kwayo wanadamu huweza kuamini mambo. Kwa uwezo wa kufikiri mtu hujifanya kuwa na kutenda ‘kana kwamba’ hivi ndivyo ilivyo (k.m. Mungu ni mwamba, Isa. 17.10; Kristo ni bwana arusi, Mt. 25:1-13). Mawazo ya mwanadamu ndio chanzo cha ufahamu wa lugha ya picha na burudani ambayo ni muhimu sana kwa mtindo wa maisha wa mtu yeyote. Kufikiria kunakusudiwa
1 Ukurasa wa 371 Utangulizi wa Somo
1
U T U M E K A T I K A M I J I
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online