Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

1 7 2 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

kuwa wakati wa msingi, muhimu, unaoendelea kubaki katika kila kitu ambacho watoto wa Mungu wa kuasili hufanya. Mawazo yanakuwa laana tu ikiwa yanafanyika ubatili. ~ C. Seerveld. “Imagination.” The New Dictionary of Theology. S. B. Ferguson, mh. (toleo tepe). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2000. uk. 331. Hakika, namna pekee ya kuyafikia mambo ya umisheni ni kwa njia ya dhana: Mungu ni bwana-arusi ambaye anawabembeleza watu ambao watakuwa bibi arusi wake na watawala wenza wake katika enzi isiyo na mwisho, na Mungu ndiye shujaa ambaye mara moja na kwa ukamilifu atamshinda shetani, kifo, na athari za laana ili kuleta utawala mpya wa haki na amani. Taswira ya bibi na arusi ni maarufu katika Agano la Kale na Agano Jipya. Katika Maandiko, uhusiano wa ndoa umetumiwa mara nyingi ili kufafanua uhusiano wa Mungu na watu wake. Israeli linaonyeshwa kama mke asiye mwaminifu wa Yehova Mungu katika Hosea, mke ambaye ameazimia kumrejesha kwenye upendo kamili na uaminifu katika Ufalme ujao. Maono haya haya yanatumika kuonyesha ukaribu na mapenzi ya kina kati ya Kristo na Kanisa katika Agano Jipya, isipokuwa kwamba Bwana mwenyewe kupitia ushawishi wa moja kwa moja na huduma ya kitume analitayarisha Kanisa kama bibi-arusi bikira anayengojea ujio wa bwana arusi wa mbinguni (2 Kor. 11:2). Yohana Mbatizaji ndiye “rafiki wa bwana arusi” sawa na msimamizi kwetu leo, ambaye alitayarisha njia ya Bwana (rej. Yn. 3:29). Yesu alitaja taswira hii ya bibi-arusi katika mafundisho yake ya ufalme (rej. Mt. 22:1-14; 25:1-13), na ilitumika kote katika mafundisho ya mitume na maono ya kinabii (2 Kor. 11:2; Efe. 5:22-24; Ufu. 21:2, 9; 22:17). Vivyo hivyo, Bwana kama shujaa wa kiungu ndiye anayekuja kuponda kichwa cha nyoka, kama ilivyotajwa katika protoevangelium ya Mwanzo 3:15. Kila sehemu ya maisha na huduma ya Kristo inaweza kueleweka katika namna ya yeye kutenda kama Mwana wa kiungu wa Adamu aliyepewa jukumu la kuwashinda maadui wa Mungu na kuuingiza utawala wa Mungu kwa furaha na nguvu. Kwa mfano, Leland Ryken anatoa muhtasari wa elimu ya Kristo ya Paulo kwa maneno haya, kwa kutumia taswira ya shujaa wa kiungu kama kanuni ya ufahamu:

1

U T U M E K A T I K A M I J I

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online