Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 7 3
Hivyo Paulo baadaye aliweza kutazama upya kifo, ufufuo na kupaa kwa Yesu Kristo katika mwangaza wa picha ya shujaa wa kiungu. Kwa mfano, katika Wakolosai 2:13-15 anahitimisha hoja yake kwa lugha ya kiushujaa wa kiungu: “Akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo” (Kol. 2:15). Katika Waefeso 4:8 ananukuu wimbo wa shujaa wa Agano la Kale (Zab. 68) na hivyo anakuzungumzia kupaa kama gwaride la ushindi: “Alipopaa juu aliteka mateka, akawapa wanadamu vipawa.” Kwa hivyo mada ya shujaa wa kiungu inatumiwa katika Agano Jipya kuelezea ushindi wa Yesu juu ya Shetani msalabani. Ingawa Shetani alishindwa, Agano Jipya pia linatambua kwamba kwa muda bado anaweza kusababisha matatizo makubwa. Kipindi cha muda kati ya msalaba na kurudi kwa Kristo ni kipindi kati ya vita vilivyohakikisha ushindi kamili na kushindwa kwa mwisho na kukoma kwa uadui. Katika wakati huu wa mpito vita vinaendelea, na kanisa linaitwa kufanya vita dhidi ya maadui wa Mungu kama vile Israeli lilivyokuwa jeshi la Mungu katika Agano la Kale. Tofauti ni kwamba silaha za kanisa ni za kiroho, si za kimwili (rej. Efe. 6:10-20). Kazi yako katika somo hili ni kuwasaidia wanafunzi kufahamu taswira hizi kama zilivyotumiwa na waandishi wa Biblia, na kuzitumia kama lenzi ili kukuwezesha kupata mtazamo mpya juu ya asili ya umisheni wa Kikristo unapotazamwa kupitia taswira hizo . Zoezi hili la ufahamu, namna hii ya kufasiri inasaidia sana katika kuujaza utajiri na nguvu umisheni wa Kikristo leo, na kuulinda dhidi ya kupunguzwa na kufanywa mbinu za kiufundi tu na kanuni za kiutendaji. Wasaidie wanafunzi wako kuelewa hisia za mafumbo na picha hizi, furaha ya karamu ya harusi, na sherehe ya adui aliyeshindwa. Picha zinawasilishwa sio tu kwa ajili ya taarifa, bali kwa ajili ya moyo na nafsi; wawezeshe wanafunzi wako kufikiri vizuri, lakini pia fanya kazi kuwasaidia kuhisi kwa kina kupitia picha hizi, kwa kuwa hiyo ndiyo sababu Bwana alitupa sisi taswira hizi. Tafadhali angalia tena malengo yaliyo hapa chini, na ukumbuke jinsi yanavyochukua jukumu kuu katika kila sehemu ya mafundisho ya darasani. Tena, moja ya majukumu yako muhimu kama Mkufunzi ~ Leland Ryken. The Dictionary of Biblical Imagery . (toleo tepe). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2000. uk. 213.
1
U T U M E K A T I K A M I J I
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online